Waislam wakiswali Swala ya Idd al- Adha ambayo imefanyika leo katika Msikiti Mkuu wa Taqwa uliopo Manispaa ya Singida.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro, akiongoza Swala ya Idd al- Adha ambayo imefanyika leo katika Msikiti Mkuu wa Taqwa uliopo Manispaa ya Singida.
Isihaka Hassan akitoa hotuba katika swala hiyo.
Katibu wa Msikiti wa Taqwa akizungumza kwenye swala hiyo.
Muhudumu wa Msikiti huo, Shafii Juma akizungumza kwenye swala hiyo.
Swala ikiendelea.
Swala ikiendelea.
Ibrahimu Ramadhani akisoma Qulaan kwenye swala hiyo.
Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye swala hiyo.
Swala ikiendelea.
Swala ikiendelea.
Dua likiombwa.
Watoto wakiwa na baba yao kwenye swala hiyo.
Swala ikiendelea.
Waumini wa dini ya kiislam wakiomba dua.
 

Na Dotto Mwaibale, Singida


SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro ametoa onyo kwa Waislam mkoani hapa kuacha tabia ya kugombea nyama na kuwataka kusaidia kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsi,ulawiti na biashara ya kuuza binadamu ambavyo vimeshika kasi na hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi.

Sheikh Nassoro, ameyasema hayo leo wakati akiongoza swala ya Idd al- Adha ambayo imefanyika katika Msikiti Mkuu wa Taqwa uliopo Manispaa ya Singida.

Alisema Mkoa wa Singida umetajwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji,ulawiti na biashara ya binadamu jambo ambalo halifurahishi na linaleta taswila mbaya kwa mkoa.
"Lakini pia kumezuka tabia kwa baadhi ya madereva wa bajaji ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ubakaji kwa wanawake na watoto,waislamu tusaidie  kufichua vitendo hivi vinaharibu sifa nzuri ya mkoa wetu," alisema.

Sheikh Nassoro alisema ili kukomesha vitendo hivyo, waislamu wanaowajibu wa kuhakikisha wanasaidiana na vyombo vya usalama likiwamo Jeshi la Polisi kwa kuwafichua wanaofanya mambo hayo ambayo yanaleta sifa mbaya kwa mkoa wa Singida.

Akizungumzia ibada ya kuchinja, Sheikh Nassoro alisema waislamu wazingatie utaratibu uliowekwa na viongozi wa mkoa ili kuepusha vurugu zisizokuwa za lazima wakati wa ugawaji wa nyama kwa wahitaji.

Alisema kila mwaka waarabu kutoka nchini Uturuki wamekuwa wakitoa takribani ng'ombe 3,000, kondoo na mbuzi zaidi ya 5,000 ambapo nyama imekuwa ikigawiwa kwa wahitaji mbalimbali wasiojiweza wakiwamo walemavu ikiwa moja ya takwa la kutekeleza ibada ya sikukuu hiyo.

Alisema mtindo wa baadhi ya waislamu kugombaniana nyama sio jambo la busara na kuwataka viongozi wa msikiti kuzingatia utaratibu uliowekwa na viongozi wa dini ngazi ya mkoa na wilaya ili kuepusha vurugu zisizokuwa za lazima kama zilizotokea jana katika baadhi ya maeneo na kusababisha Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kulazimika kupiga mabomu ili kuwatawanya.

Katika hatua nyingine Sheikh Nassoro ametumia ibada hiyo kuwaimiza waislam wote kujitokeza kwa wingingi kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23 mwaka huu na kueleza kuwa yeye pamoja na Mufti Mkuu wa Tanzania , Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally kuwa watakuwa wa kwanza kuhesabiwa.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: