MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki ibada ya kusimika jimbo jipya la Ikungi pamoja na kumsimika Askofu jimbo Mchungaji Jeremiah Mpepho katika ibada iliyoongozwa na askofu mkuu wa Kanisa la FPCT Tanzania Mchungaji Stevie Robert Mulenga


Ibada hiyo imehudhuriwa pia na viongozi wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry Muro, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa, mwenyekiti wa halmashauri ya Ikungi Ali Mwanga pamoja na mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu na madiwani wa halmashauri ya Ikungi


Akizungumza Julai 23,2022,wakati wa usimikaji wa jimbo,Mtaturu  amempongeza sana Askofu Mpepho kwa kupata  baraka kushika nafasi hiyo na kumuelezea kuwa ni mtu mnyenyekevu.


Amewaomba wachungaji wa chini yake wamtunze na kumpa ushirikiano.


"Niwaombe viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan ili kuendelea kuwa na amani,"amesema.


Kwa upande wake Askofu Mkuu wa FPCT Mulenga amepongeza ushirikiano uliopo baina ya kanisa na serikali kuanzia ngazi ya Taifa mpaka wilaya na kusisitiza ushirikiano huo ndio umechangia kupatikana kwa jimbo la Ikungi 


Awali wakizungumza katika ibada hiyo Mkuu wa wilaya ya Ikungi na mbunge wa Singida Magharibi Kingu wamesema Ikungi imeanza kufunguka hivyo kuwataka wananchi kutumia fursa ya kuanzishwa kwa jimbo hilo ili kuweza kupata huduma za kiroho kwa mfumo ulio bora zaidi.


Katika kuunga mkono wito wa kuchangia mfuko wa jimbo jipya mbunge Mtaturu amechangia Sh.Milioni 1.5 na pikipiki 2,mbunge Kingu amechangia Sh Milioni 1,mwenyekiti wa CCM wilaya amewapatia kanisa Kiwanja cha kujenga kanisa,Mkuu wa wilaya laki 5 ,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Ally Mwanga amechangia Sh laki 2 na madiwani wa kata za Unyahati,Isuna na vitimaalum Ikungi walichangia kila mmoja Sh 50,000.


Share To:

Post A Comment: