MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekabidhi ukumbi wa Tawi la simba baada ya kutoa ufadhili wa mabati 37,mbao za upauaji za Sh laki 6,viti 20 na meza 2 zenye thamani ya Sh. 437,000 vitu hivyo amevikabidhi mbele ya mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry Murro. 


Akimkabidhi mwenyekiti wa tawi la simba Ikungi John Chao, Mtaturu amesema simba ni timu kubwa hivyo kama Mbunge ameona wawe na ukumbi wa kuangalizia mpira na kujadiliana maendeleo ya timu. 


"Niwaombe wanasimba kuwa wamoja ili kuimarisha uhai wa timu yetu,"amesema.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya amempongeza Mbunge Mtaturu kwa moyo wake wa kujitolea kwa ajili ya jamii. 


Amemuhakikishia kuwa atafuatilia utunzaji wa ukumbi huo ili iwe ni sehemu ya kukutania wapenzi wa michezo.


Mwenyekiti wa Tawi la simba ndugu John kwa niaba ya wapenzi wa simba amemshukuru sana Mbunge kwa uzalendo wake wakujitolea mchango huo mkubwa na kuahidi kuutunza ukumbi pamoja na runinga aliyoitoa mapema mwaka huu ili kuangalizia michuano mbalimbali ya ligi kuu na ligi za kimataifa ikiwemo kombe la dunia.


Share To:

Post A Comment: