Mfamasia Kituo cha Afya Makorora Tanga Bi.Gloria Urio akionesha baadhi ya vifaa tiba kwaajili ya upasuaji walivyokabidhiwa na Bohari ya Dawa hivi karibuni baada ya kuwa na changamoto ya vifaa tiba hivyo na kutokutoa huduma ya upasuaji kwenye kituo hicho cha Afya Mkoani Tanga.
Vifaa tiba kwaajili ya upasuaji vilivyopo katika kituo cha afya Makorora mkoani Tanga vikiwa tayari kwaajili ya kutoa huduma ya upasuaji. Vifaa hivyo vimekabidhiwa hivi karibuni na Bohari ya Dawa (MSD). Vifaa tiba kwaajili ya upasuaji vilivyopo katika kituo cha afya Makorora mkoani Tanga vikiwa tayari kwaajili ya kutoa huduma ya upasuaji. Vifaa hivyo vimekabidhiwa hivi karibuni na Bohari ya Dawa (MSD). Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack akizungumza na baadhi ya watumishi wa MSD (hawapo picha) mara baada ya kutembelea kituo cha afya cha Makorora kilichopo mkoani Tanga Mfamasia Kituo cha Afya Ngamiani mkoani Tanga, Bw.Michael Mrosso akiangalia vifaa tiba ambavyo wamekabidhiwa na MSD hivi karibuni Jenerata ambalo litatumika kuzalisha umeme pindi umeme wa kawaida unapotokea kukatia katika Kituo cha Afya Ngamiani mkoani Tanga. Jenereta hilo limekabidhiwa na Bohari ya Dawa (MSD) hivi karibuni.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, TANGA

SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imepongezwa kwa kuwezesha kukabidhi vifaa tiba katika vituo vya afya mkoani Tanga, vifaa ambavyo vilikuwa changamoto katika utoaji huduma vituoni humo.

Akizungumza leo Julai 17,2022 katika mahojiano maalumu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack amesema walipokea vifaa vya chumba cha upasuaji ikiwemo kitanda cha upasuaji, mashine ya dawa ya usingizi na taa zinazotumika wakati wa upasuaji amesema vifaa hivyo ni msaada mkubwa katika kituo hicho kwani awali kulikuwa na changamoto kwenye hutoaji huduma.

"Awali tulikuwa hatufanyi upasuaji kabisa kwa hiyo tulivyopokea fedha kwa ajili ya ukarabati majengo ya kufanyia upasuaji tulifanya hivyo na baadae vifaa vililetwa na MSD na kuanza kutoa huduma za upasuaji". Amesema Dkt.Angelina

Amesema baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo walianza kutoa huduma ya upasuaji mbalimbali wa mama wajawazito pamoja na upasuaji mdogo kwani hapo awali walikuwa wanawapeleka wagonjwa hospitali ya Bombo kwa sababu huduma hiyo haikuwepo hapo kituoni. "Kwa ujio wa vifaa hivi imerahisisha mama mjamzito akipata changamoto moja kwa moja tunaweza kumpa huduma ya upasuaji na tunaokoa maisha ya mama pamoja na kichanga". Amesema.

Pamoja na hayo Dkt.Angelina amesema walikabidhiwa pia na jenereta kwa ajili ya hospitali hiyo lakini wakaamua kuwasiliana na ofisi ya mganga mkuu ili waweze kuichukua na kuikabidhi kwenye vituo vingine ambavyo havina jenerata kwa sababu kituo hicho kilikuwa na jenerata ambayo walikuwa wameshanunua awali.

Ameeleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika kituo hicho ni nzuri kwani kwa sasa dawa muhimu zinapatikana kwa asilimia 90 na wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi .

Naye Mfamasia wa Kituo cha Afya Ngamiani mkoani humo, Bw. Michael Mrosso amesema walipokea vifaa tiba kwa aajili upasuaji pamoja na jenerata, vifaa ambavyo vilikuwa ni kilio chao kwa muda mrefu.

Amesema wataendelea kujitahidi kutoa huduma bora kwa kuwa kuna vifaa bora ambavyo wamekabidhiwa na serikali kwa ajili ya kuwahudumia wananchi
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: