Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mamlaka hiyo muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara-SabaSaba barabara ya Kilwa, Temeke jijini Dar es salaam. TCRA inashiriki Maonesho hayo kwa kutoa elimu kwa watumiaji huduma za Mawasiliano. Picha: TCRA
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk.Jabiri Bakari akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Ufunguzi wa Maonesho ya 46 ya Maonesho ya Biashara Kimataifa Sabasaba , Jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiingia na kutoka kwenye banda la TCRA katika Maonesho ya Viwanda na Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam kupata elimu,huduma na msaada wa huduma za Mawasiliano. Picha: TCRA
Mtambo wa kukagua Masafa ya Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Mtambo huu upo katika banda la maonesho ya biashara-SabaSaba barabara ya Kilwa. TCRA wanakukaribisha ujifunze namna mtambo huo unavyofanya kazi. Picha: TCRA


Post A Comment: