Wana Ndoa Bosco Chailla na mkewe Tusajigwe Chailla (kulia) wakiwa katika upendo wa dhati na amani kabla ya kuanza kudaiana talaka mahakamani ili waweze kugawana mali walizochuma wakiwa pamoja.

Wanandoa hao wakiwa na furaha kabla ya kuanza kudaiana talaka.
Wanandoa hao wakiwa wameshikana mikono kuonesha upendo wa hali ya juu. 
Mama Tusajigwe akiwa amelazwa Hospitali akipatiwa matibabu na moja ya sababu anayodai imechangia kuachana na kudai talaka ni mume wake kushindwa kumuhudumia akiwa mgonjwa.

 

Na Mwandishi Wetu, Manyoni.

 

MGOGORO wa kifamilia kati ya Bosco Chailla na mkewe Tusajigwe Chailla (Mwanjala) umeingia katika sura mpya baada ya kufikia hatua ya kuwatimua watoto wao kulala ndani ya nyumba iliyopo Kijiji cha Solya wilayani Manyoni mkoani Singida. 

Wanandoa hao ambao katika miaka zaidi ya 40 ya ndoa yao wamefanikiwa kujenga nyumba za kuishi na vibanda vya biashara jijini Dar es Salaam na wilayani Manyoni, ugomvi wao umeshika kasi zaidi baada ya kila mmoja kufungua kesi ya kuomba talaka ili kuachana. 

Mwanamke ndiye alikuwa wa kwanza kufungua kesi mahakamani kuomba talaka kwa mwanaume ili waweze kugawana mali lakini baadaye aliamua kufuta kesi hiyo. 

"Niliamua kuomba talaka baada ya kunidhalilisha wakati naumwa na kulazwa katika hospitali ya Benjamini Mkapa," alisema Tusajigwe.  

Baada ya kufuta kesi hiyo, mwanaume naye ameamua kufungua kesi namba 640/2022 ya kuomba talaka kwa mke wake ambayo inaendelea hadi sasa katika mahakama ya mwanzo Temeke jijini Dar es Salaam. 

Katika mali wanazomiliki, nyumba ya kuishi iliyopo kijijj cha Solya kitongoji cha Ushola ndio imekuwa na mvutano mkubwa ambapo mwanaume anadai nyumba hiyo ni mali ya baba yake mzazi na sio miongoni mwa mali walizochuma na mke wake Tusajigwe Chailla. 

Katika nyumba hiyo ambayo ukiachilia ndugu zake Bosco wanaoishi hapo lakini pia watoto wao Beatrice Bosco na Boniface Bosco walikuwa wakiishi hapo lakini mwezi uliopita walitimliwa hapo na hivi sasa wanahangaika hawana mahali pa kuishi. 

Inadaiwa mzee Bosco alipiga simu kwa mdogo wake aitwaye Benny na kumwagiza afunge milango ya vyumba walivyokuwa wakiishi watoto hao pamoja na mama yao na watafute sehemu nyingine ya kuishi. 

"Tulifungiwa nje mimi na watoto wangu na hadi nakuambia hivi sasa ndugu mwandishi nguo zangu ziko ndani ya chumba nilichokuwa naishi," alisema Tusajigwe ambaye alionekana kuwa na majozi makubwa kutokana na mgogoro wa ndoa yao. 

Uamuzi huo wa Bosco ulitokana na kwamba watoto hao tangu mwanzo wa ugomvi huo wamekuwa upande wa mama yao hatua ambayo baba yao (Bosco) anawaona maadui kwake. 

Vyumba walivyokuwa wanaishi watoto hao vilifungwa Juni 22, mwaka huu saa 3:00 usiku ambapo zoezi la kuvifunga linadaiwa kusimamiwa na Benedick Chailla, Rose Chailla na Regina Chailla, mwenyekiti wa kitongoji na mwenyekiti wa kijiji. 

Kabla ya tukio la kufungwa vyumba hivyo, Tusajigwe Bosco Chailla (mke wa Bosco) alikwenda kijiji cha Solya akitokea Jijjini Dar es Salaam ambapo inadaiwa alipofika katika nyumba hiyo alitaka kulala hapo na ndipo ugomvi ulizuka. 

Kufuatia ugomvi huo ndugu zake Bosco, ambao ni Rose Chailla ambaye ni Mama Mchungaji Ruvumbi na Regina Chailla waliwekwa ndani katika kituo cha polisi Manyoni kuanzia Juni 22 hadi Juni 23 mwaka huu wakidaiwa kuvamia nyumba hiyo iliyopo Solya. 

Kufuatia ugomvi huo ambao unahatarisha amani, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Manyoni, aliwaita wanafamilia hao na kukubaliana mambo kadhaa ili kuepusha ugomvi ambao unahatarisha kumwagika damu katika familia hiyo. 

Makubaliano ni kwamba mama yaani Tusajigwe Chailla asiishi katika nyumba iliyopo Solya inayong'ang'aniwa na kila mmoja na badala yake akaishi Dar es Salaam ili kusubiri maamuzi ya mahakama katika kesi ya kuomba talaka iliyopo mahakama ya mwanzo Temeke.ia, vibanda 15 vya biashara ambavyo vimekodishwa kodi ya wapangaji iwe inachukuliwa na  Bosco ambapo Tusajigwe asiwe anahusika. 

Aidha, mzee Bosco awajibike kumpatia Sh. 1,000,000 kila mwezi mke wake yaani Tusajigwe hadi hapo kesi iliyopo mahakamani itakapomalizika na suala la kugawana mali litakapofanyika. 

Wakati wa usuluhishi huo, Bosco alikubali mbele ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) kwamba kesi ya talaka itakapoisha yuko tayari kugawana mali walizochuma na mke wake ili baada ya hapo kila mmoja aishi kivyake. 


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: