Na John Walter-Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameonesha kwa vitendo azma yake ya kuinyanyua sekta ya kilimo na wakulima ili izidi kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi.

"Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia kwenye Nchi yetu hii ni bajeti ya kwanza inaletwa na Serikali na hakuna mtu analalamika kwamba ni ndogo hapa nimpe pongezi Rais Samia kwa hakika ameonesha kuwajali watanzania kwa vitendo, maslahi ya wakulima,wafugaji na wavuvi"alisema 

Amesema bajeti hiyo italeta mapinduzi makubwa kwenye sekta mbalimbali hivyo kupanua wigo kwa walipa kodi na kuongeza malighafi za viwandani.

"Niipongeze Serikali kwa kuongeza bajeti ya Kilimo hadi kufikia Sh Bilioni 751,kundi kubwa la vijana linakwenda kushiriki Kilimo" alisema Sillo

Aidha amewaambia wakazi wa Jimbo la Babati Vijijini kuwa bajeti hiyo itagusa sekta ya afya ambapo vituo vya afya vya Madunga,Bashnet na Ayasanda na Gidas vitakwenda kukamilika pamoja na Zahanati ambazo hazijakamilika.

Serikali  imewasilisha bungeni bajeti yake kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo jumla ya shilingi trilioni 41.48 zinatarajiwa kutumika. Shilingi trilioni 28.02, zitatokana na vyanzo vya ndani.

Share To:

Post A Comment: