Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mhe.Elibariki Immanuel Kingu

 

 Thobias Mwanakatwe na Dotto Mwaibale, Singida

 

MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Mhe.Elibariki Immanuel Kingu,anatarajia kuanza ziara ambayo itadumu kwa mwezi mmoja katika kata 15 za jimbo hilo.

Kingu katika taarifa yake leo kwa vyombo vya habari, alisema ataanza ziara hiyo Julai 20 na kuihitimisha Augosti 20, mwaka huu ambapo katika ziara hiyo atafanya mikutano ya hadhara na wananchi wa kata hizo.

Alizitaja kata ambazo atafanya mikutano ya hadhara kuzungumza na wananchi kuwa ni kata ya Iyumbu, Mgungira, Mwaru, Igombwe, Irisya, Sepuka, Minyughe na Mtunduru.

Kata nyingine ni Kituntu, Puma,Ihanja, Iseke,Iglansoni, Muhintiri na Makilawa

Alisema mikutano hiyo ambayo itakuwa mikubwa,  atatumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi mambo yaliyopitishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha 2022/2023, kuwaeleza mipango ya Serikali na kuchukua maoni ya wananchi kila kata.

"Katika mikutano hiyo ya hadhara nitawaeleza wananchi wangu mageuzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika nyanja zote tangu ameshika madaraka hayo," alisema Kingu.

Aidha, alisema katika mikutano hiyo atawahamasisha wananchi kujitokeza kujiandaa kuhesabiwa katika zoezi la sensa ambalo linatarajia kufanyika Agosti 23, mwaka huu nchi nzima.

"Wananchi wote naomba tujiandae kuhudhuria kwa wingi kujua nini  mwakilishi wenu amefanya katika kipindi cha mwaka huu," alisema.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: