Hali isiyo ya Kawaida imeibuka katika kata ya Majengo Wilayani Monduli Baina ya vijiji vya Losirwa,Majengo ,Mungere,na Baraka baada ya wakulima kushikilia Mifugo ya wafugaji kwa Madai ya kuwaingiza kwenye Mashamba yao .


“Nilipigiwa simu nikiwa Naelekea Mswakini kwenye Mazishi ya wale watoto 5 wa familia moja , ikabidi nifike na kuwapa pole familia , ndugu na Majirani kwanza ili niweze kufika na hapa Majengo kutokana na taharuki baina ya wakulima na wafugaji  ninachoweza kusema MARIDHIANO ndiyo Njia pekee ya kupata Suluhu ya kudumu juu ya mgogoro huu naomba viongozi wa Eneo husika kukaa pamoja na Kuweka MARIDHIANO ili kutafuta Suluhu ya kudumu sisi wote ni ndugu tunategemea”.mbunge Fredrick Lowassa 


Awali wafugaji wakati wakizungumza mbele ya Mbunge huyo wamemuomba mbunge huyo , kuomba kuachiiliwa kwa ndugu zao walioshikiliwa na polisi ili waweze kusema changamoto zao ndipo mbunge huyo kuomba kuachiliwa kwa mwananchi na polisi Kumruhusu kuachiliwa, na kuomba kufanyika kwa Maridhiano ya kudumu .


Nao baadhi ya wakulima wamesema Hawataachia Mifugo Hiyo hadi wapate Suluhu ikiwemo pia kulipwa Fidia ya Mazao yao yaliyoharibika.

Share To:

Post A Comment: