WATUMISHI wa chama cha Mapinduzi (CCM) makao makuu na Jumuiya zake wamepiga kura ya kuchagua viongozi ambao wataiongoza Mapinduzi Sports klabu.


Viongozi waliochaguliwa ni Mwenyekiti,makamu mwenyekiti, katibu mkuu katibu mkuu msaidizi, mweka hazina mjumbe wa mkutano mkuu na wajumbe wa kamati tendaji.


Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Mapinduzi Sports Club Zakayo Kishiwi ilieleza kuwa katika uchaguzi huo wajumbe wamemchagua Kajoro Vyohoroko kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo,Annael Samweli Makamu mwenyekiti, na Neema Mfugale kuwa katibu Mkuu.

“Viongozi wengine waliochaguliwa ni katibu msaidizi Jumanne Mzee na Eunice Malya amechaguliwa kuwa mweka hazina.


Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwa wajumbe walimchagua Hamis Hilali kuwa mjumbe wa mkutano mkuu na kuwapitisha wajumbe wa kamati tendaji ambao ni Bushuru Mohamed, Elizabeth Muhina, na Marry Ngerangera.


Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa mwenyekiti huyo aliahidi kuifufua mapinduzi sports klabu kivingine katika michezo yote .

 “Uchaguzi wa viongozi hao ulifanyika Julai 8 mwaka huu katika ukumbi wa NEC uliopo CCM makao makuu chini ya usimamizi wa wa mwenyekiti wa uchaguzi Wilson Nkambaku,”ilieleza.

Share To:

Post A Comment: