Shirika la Msalaba mwekundu (REDCROSS) Tanzania limetoa Msaada wa Fedha Shilingi Millioni 23 kwa Waathirika wa Maafa ya mifugo kwa kaya 114 katika kijiji cha Idonyoonaado kata ya Mfereji Wilayani Monduli Mkoani Arusha.


Akizungumza Rais wa Shirika hilo (REDCROSS TANZANIA) David Mwakiposa Kihenzile Ambaye Ndiye Mgeni rasmi katika zoezi la Ugawaji wa Fedha hizo amesema wamejikita hasa kutoa Misaada za kibinadamu kabla na baada ya Maafa , Ambapo Msaada huo unalenga Kaya zilizoathirika na Maafa ya Mifugo Mwaka jana .


Kihenzile ameongeza kuwa  Wanagusa Familia zilizoathirika na Ukame, Ambapo jumla ya vifo vya Mifugo ni Punda zaidi ya elfu 2 Ng’ombe zaidi ya elfu 41,Mbuzi zaid elfu 34, na Kondoo zaidi ya elfu 54, kwa Wilaya ya Monduli, na kusema  pamoja na kutoa Fedha taslim wametoa Elimu ya kupinga ukatili, Madumu ya maji na vidonge vya kutibu maji , na Jumla ya Fedha zilizotolewa kwa Mikoa  ya Manyara na Arusha ni Jumla ya Millioni 216 kwa kaya elfu Moja na Mia mbili (1200).


Fredrick Lowassa ni Mbunge wa jimbo la Monduli ambaye ndiye mwenyeji Katika ziara ziara hiyo Amemshukuru Rais wa Redcross Tanzania kwa Kufika idonyonaado, na Kusema mchakato huo ni wa kitaalamu , Miundombinu ya idonyonaado ni changamoto kupatikana kwa maendeleo na kusema Tayari shule ya Msingi imeshajengwa na kuahidi kupatikana kwa Huduma mbalimbali za kijamii katika kijiji hicho kupitia kwa wafadhili, Serikali na Jamii kwa ujumla.


Kwa Upande wa Mnufaika wa  Msaada huo Putian Memusi Amesema Fedha hizo atazitumia kununua chakula cha Mifugo (pumba) na kuwashauri wanufaika wengine kutumia kwa Malengo na si kuchezea.










Share To:

Post A Comment: