Jukwaa la taifa la wadau wa udhibiti wa maafa kwa ajili ya kithibitisha mpango wa taifa wa pamoja na mkakati wa mawasiliano wakati wa dharura limekutana leo jijini arusha kwa lengo la kujadili namna bora ya kujikinga na maafa

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo ameishukuru benki ya dunia kwa kuwezesha wataalam na rasiliamali fedha kuhusisha nyaraka hizi muhimu  ambazo zitajadiliwa katika jukwaa hili 

Amesema Ofisi ya Waziri Mkuu katika kutekeleza Sheria ya Usimamizi wa Maafa Sura ya 242 na Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa itaendelea kuimarisha uratibu wa shughuli za udhibiti wa maafa kwa kuhakikisha uwepo wa mifumo thabiti katika ngazi zote. Hivyo, Jukwaa la Taifa la Wadau wa Udhibiti wa Maafa ni chombo muhimu kilichoanzishwa kwa mujibu wa Sheria hii kwa ajili ya kuhakikisha ushiriki wa wadau katika shughuli za udhibiti wa maafa nchini.

Aidha amesema nchi kwa sasa imekuwa ikishuhudia kuongezeka kwa matukio ya majanga ambayo yamekuwa yakisababisha maafa na kuathiri mfumo wa kawaida wa maisha katika jamii

Amefafanua kuwa Maafa haya yamekuwa yakisabibisha madhara mbalimbali ikiwemo vifo, ulemavu wa kudumu, upotevu na uharibifu wa mali na mazingira. Madhara mengine ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umma na binafsi iliyotumia gharama kubwa kuijenga

 Aidha, nalishukuru Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambalo limewezesha kufanyika kwa Jukwaa la Taifa la Wadau wa Udhibiti wa Maafa ili kutoa fursa kwa wadau.



















Hivyo, mpango unatoa fursa kwa taasisi na wadau wote kushiriki katika shughuli za upunguzaji wa vihatarishi vya maafa na kutoa huduma za misaada ya kibinadamu inayohitajika wakati wa maafa.


Share To:

Post A Comment: