Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kupitia ubunifu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufanikisha kupatikana kwa Mkopo wa Ahueni ya UVIKO-19 kiasi cha Shilingi Trilioni 1.3 ambapo kwa Sekta ya Afya Mhe. Rais Samia Suluhu alitoa kiasi cha Shilingi Bilioni 466.8 ambazo zinakwenda kugusa maisha ya Mtanzania kwa kuboresha huduma za afya nchini.


Mheshimiwa Ummy amesema kupitia fedha hizo Serikali imeweza kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini pamoja na kusogeza huduma za vipimo vya kibingwa katika ngazi ya Mkoa ili kumuwezesha Mtanzania kupata huduma bora za afya nchini.

Share To:

Post A Comment: