Mwanafunzi wa Chuo cha VETA cha Mafunzo ya Hoteli na Utalii (VHTTI) kilichopo Njiro mkoani Arusha Happiness Michael akiwa ameshika ndizi Kitarasa ambayo ikichanganywa na mbaazi inatengeza vyakula ambavyo vinatibu magongwa mbalimbali yakiwemo ya sukari, pasha , kuongeza kinga ya mwili pamoja na kuimarisha afya ya akili kwa mtoto.Mwanfunzi huyo yuko kwenye banda la VETA katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.

Happiness Michael ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha VETA ch Mafunzo ya Hoteli na Utalii kilichopo Njiro mkoani Arusha akionesha unga unatokana na ndizi kitarasa ambayo inatumika kutengeneza aina mbalimbali za vyakula.

Baadhi ya wanafunzi na walimu wa Chuo cha VETA cha Mafunzo ya Hoteli na Utalii Njiro mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kwenye banda la VETA.



 CHUO cha VETA cha Mafunzo ya Hoteli na Utalii(VHTTI) kilichopo Njiro mkoani Arusha ambacho kinamilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)kimekuja na ubunifu wa mazao ya ndizi kitarasa na mbaazi kutengeza vyakula ambavyo vinatumika kutengeneza vyakula ambavyo ni tiba ya kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kisukari na presha.

Akizungumza kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba Mwanafunzi anayesomea katika chuo hicho Happiness Michael amesema kwa mwaka huu katika maonesho hayo wamekuja na ubunifu wa mapishi kwa kutumia ndizi kitarasa na mbaazi.

“Sisi na walimu wetu katika maonesho ya mwaka huu tumekuja na ubunifu wa mazao ambayo ni ndizi na mbaazi na ndizi , hii ndizi ambayo tumeileta hapa iko tofauti na ndizi zingine, hivyo tumeamua kuchagua ndizi Kitarasa na mbaazi ni kwasababu mazao hayo yalikuwa hayapewi kipaumbele katika mlo wa binadamu.

“Kwa hiyo sisi tumechukua hiyo fursa na tulilenga kwa watu ambao hawatumii ngano kwa hiyo tumetumia ndizi kitarasa pamoja na mbaazi kutengeza baadhi ya vyakula ama vyakula vyote vinavyokuwa vinatengenezwa na ngano, mfano mkate , maandazi ,biskuti, keki na hiyo sio moja kwa moja mtu anakula tu lakini anakuwa anapata tiba.Mtu anapotumia ndizi kitarasa na mbaazi anakuwa anatibu kisukari , presha, mwili wenye kujaa mafuta na vile vile kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo la kinga za mwili zinakuwa zinashuka.

“Na hata watoto zinakwenda kujenga afya ya akili, ndizi ya kitasara yenyewe iko tofauti na ndizi nyingine na yenyewe kinachoangaliwa ni ule utomvu ambao ndio tiba yenyewe na ndio maana tukaamua kuchagua ndizi kitarasa.Hata wanaotaka kuacha kuvuta sigara ni vema wakatumia ndizi kitarasa na mbaazi .

“Hii ndizi unaweza kutumia ikiwa mbivu, ikipikwa ,na unga, lakini kwa sisi tulikuwa tunalenga kutumia unga , hivyo tulikuwa tunachukua ndizi kitarasa kisha tunamenya tunaanika na tukishaanika tunakwenda kusaga na kupata unga kwa ajili ya matumizi ya kutengeza vile vitafunwa.Hii ndizi na tangu enzi na enzi na kule Kilimanjaro zamani ilikuwa inatumika wakati wa njaa,”amesema.

Wakati huo huo, amesema chuo chao mbali ya kuja na ubunifu wa mazao hayo ,wamekuw wakielezea kozi ambazo zinafundishwa katika chuo chao ambacho kipo kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tatu.

Ametaja baadhi ya kozi ni uokaji mikate, keki na mapishi ya vyakula, mapambo na upambaji wa kumbi za starehe, mafunzo ya kompyuta na mbinu za uandaaji Cocktail.

Kozi nyingine ni ya usafi wa majengo na maeneo ya wazi, huduma kwa wateja , mbinu za ujasiriamali, usimamizi wa shughuli za mapokezi na vyumba, uhudumu na uuzaji wa chakula na vinywaji, uaandaji na upishi wa chakula , utaalamu wa uongozaji watalii pamoja na uandaaji na uendeshaji wa safari za watalii.

Share To:

Post A Comment: