Raisa Said,MUHEZA.

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga imemuhukumu kifungo cha Maisha jela, Mgaya Mngazija mwenye Umri wa Miaka (39) Mkazi wa Kijiji cha Kicheba B baada ya kupatikana na hatia ya Kumlawiti Mtoto wa Umri wa Miaka (6).


Akisoma hukumu hiyo Hakimu Yusufu Zahoro Mahakamani hapo baada ya Mahakama kusikiliza Mashahidi 7 kutoka upande wa Mshitaki akiwemo Dkt,  na Mashahidi 5 kutoka upande wa utetezi akiwemo Mama mzazi wa Mlalamikiwa ambae pia ni Bibi wa Mtoto huyo amesema anatoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa Watu wengine wenye tabia ya vitendo kama hivyo na wale wanaofikilia kutenda Makosa kama hayo iwe fundisho kwao.


Aidha Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Hadija Chanyendo amepongeza Wazazi wa Mtoto kwa hatua ambayo wameifanya licha ya kuangalia kuwa Mtuhumiwa ni Baba Mkubwa wa Mtoto huyo na kuto kumaliza kesi hiyo kifamilia.


Nae Baba Mkumbwa wa Mtoto huyo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama baada ya hukumu kutolewa amepongeza Mahakama kwa kutoa adhabu hiyo iliiweze kuwa fundisho kwa Wazazi kuona namna wanavyoweza kutetea haki za Watoto wao.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: