Na John Mhala, Arusha

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, julai 3 mwaka huu anatarajiwa kuziongoza taasisi kadhaa zinazohusiana na Kiswahili Nchini, katika uzinduzi wa kitabu cha ziada cha Riwaya ya Kwaheri katika tukio linalotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa NSSF Mafao House ulipo Ilala Boma.

Katika siku hiyo ya Uzinduzi ni siku maalumu ya Mjue Mtunzi iliyoandaliwa na Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI) ikishirikiana na Mdhamini Mkuu Elite Bookstore.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Arusha leo ,Mwandishi wa Kitabu cha Kwaheri,Hassan Ally Hassan alisema mbali ya Waziri Mkenda,taasisi zinazohusiana na Kiswahili, zinazotarajiwa kushiriki katika hafla hiyo, ni pamoja na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA), Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, COSOTA, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Wahadhiri mbalimbali wa Vyuo Vikuu pamoja na Wasomaji na wapenzi wa kazi za fasihi ya Kiswahili Nchini 

Hassani, alisema Hafla hiyo inakadiriwa kuwa na washiriki zaidi ya 300 watakaoshiriki moja kwa moja ukumbini katika uzinduzi huo. Vilevile aliongeza kuwa hafla hii itahusisha utoaji wa ngao kwa watunzi watatu wa UWARIDI kwa kutambua jitihada zao katika uandishi wa vitabu vya Riwaya Nchini.

Aidha, alisema lengo la kuandika kitabu cha Kwaheri ni kuleta mabadiliko ya kifikra katika jamii hasa kwa wanafunzi  wa shule za sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu wanaosoma fasihi kwa kuja na riwaya ya usasa ambayo inawawezesha wasomaji kupata maarifa halisi kupita kazi ya fasihi ili kuchochea ufanisi mkubwa wa maendeleo kwenye sekta mbalimbali Nchini.

“Riwaya hii inaelezea mapito ya kiutawala na masuala ya kijamii yanayoibuka na kuleta tafakuri kwa wanajamii kuhusiana na utamaduni; matakwa ya vijana yanayogongana na yale ya wazee na matarajio ya jamii; Suala la utaifa na matatizo yake. Pia kimesheheni masuala la elimu, sayansi, siasa, jografia na utalii, tiba, uzalendo, umaskini, magonjwa, mapenzi na ndoa, rushwa, uongozi mbaya, umuhimu wa elimu pamoja na ufujaji wa mali za umma” alisema

Hata hivyo, alisema aliandika kitabu hicho, ili kutoa mchango wake wa kuusaidia mfumo wa elimu wa Tanzania, kutokana na mapungufu yaliyoko kwa kuwa na Riwaya zinazotumika sasa hivi zimeandikwa miaka mingi iliyopita hivyo kuna baadhi ya mambo hayaakisi mahitaji ya ulimwengu wa sasa pamoja na kuja na aina mpya ya uandishi wa fasihi unaojikita kwa msomaji kupata maarifa halisi na kupata mbinu mbadala za kukabiliana na changamoto zilizopo katika jamii yake kupitia kazi za fasihi.

Mwandishi wa kitabu hicho alisema amefanya kazi katika sekta ya elimu kwa zaidi ya miaka 17 sasa, amesoma fasihi ya kiswahili kuanzia sekondari hadi chuo kikuu na amepokea Cheti cha Ithibati kutoka wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2021 kinachoidhinisha  kitabu hiki kuwa kitabu cha ziada kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania.

Alisema kufuatia hali hiyo anaamini kitaweza kuleta mabadiliko ya fikra na kuwa katika mwenendo bora wa kuwa na watu wenye tija katika Taifa.

Alisema kwenye riwaya hii iliyoandikwa kwa mtindo wa safari wasomaji watapata fursa ya kufanya utalii wa ndani na kufahamu vivutio vilivyoko katika nchi yetu, rasilimali na jografia yetu ikiwamo Hifadhi za Taifa, mbuga za wanyama, sura ya nchi ya mikoa mbalimbali.


Pia alisema baada ya kukizindua atarejesha shukrani zake kwa jamii kwa kutoa nakala moja ya Riwaya ya Kwaheri kwa Maktaba zote za shule za sekondari za serikali za Jiji la Arusha ikiwa ni moja ya jitihada za kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Muda mrefu 2011/12 hadi 2024/25, ambapo Serikali imelenga kujenga jamii iliyoelimika na yenye kupenda kujielimisha.

Alisema chimbuko la kuanza kukiandika kitabu hicho, ulianzia katika kazi za darasani wakati akisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aidha, katika kuhakikisha anaandaa riwaya bora alihak

Share To:

Post A Comment: