Mtendaji Mkuu wa Tanroads Rogatus Mativila akitoa Maelezo ya mchoro wa mizani kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa Wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mizani ya Kimokouwa Wilayani Longido Mapema Jana picha zote na Ahmed Mahmoud Longido



Pichani Katikati ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela na Mbunge wa Longido na Naibu Waziri wa Madini DKT.Stephen Kiruswa Wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mizani ya Kimokouwa Wilayani Longido 


Na Ahmed Mahmoud


WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amewataka watendaji wa TANROAD wanaofanyakazi Kwenye mizani ya kupima uzito wa Magari  kujitathimini katika utendaji wao kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya ya wamiliki wa Magari kutotendewa haki kwenye mizani mbalimbali hapa nchini.


Alisema hayo leo  kwenye uzinduzi wa mizani mpya ya kisasa iliyopo eneo la kimokouwa wilaya ya Longido iliyojengwa kwa fedha za ndani kwa asilimia 100 na kugharimu sh billion 14.718.


"Najiuliza kwa Nini mizani A ikipima inapata Tan 10 lakini gari hili hili likifika mizani B anaambiwa ni Tan 11 au zaidi,kwa Nini,naomba mjitafakari malalamiko ni mengi,madereva wananipigia simu Kila Leo wakilalamika" alisema 


Aidha alieleza kuwa kumekuwepo na watendaji wachache wa TANROAD wanaojihusisha na masuala ya rushwa katika utendaji kazi na Hali hiyo upelekea kuwaandikia faini waliozidisha mzigo baada ya kushindwa kukubaliana Kama ilivyo matarajio yake.


" Unakuta Mtendaji kaomba rushwa laki moja yule mtu Hana hivyo anapakiwa pembeni na kuandikiwa faini,ukiletewa Ile faini ukitizama na thamani ya gari unakuta gari Ina thamani ya sh.milion 10 lakini faini aliyoandikiwa ni sh million 30 ataitoa wapi?" amesema


Katika hatua nyingine aliwataka wamiliki wa Magari kuzingatia sheria za nchi ikiwemo sheria za barabara kuepuka kuzidisha mizigo kwenye magari ili kuepukana na faini zisizo za lazima,lazima mtambue sheria ni Kali na ni msumeno,hata Kama utapunguziwa faini ila ni lazima utalipa faini.


Alisema katika kuzingatia utunzaji wa miundombinu ya barabarani hapa nchini,serikali imezingatia kujenga vituo vya kupimia uzito wa mizigo iliyobebwa kwenye magari lengo likiwa ni kuthibiti uharibifu wa barabara zetu na kupunguza ukarabati wa Mara kwa Mara kwani fedha ni nyingi hutumika.


" Miongoni mwa vitu vinavyo haribu barabara zetu ni pamoja na umwagaji wa mafuta barabarani,uzibaji wa mitaro pamoja na uzidishaji wa mizigo kwenye magari,hivyo nawaagiza TANROAD kutoa elimu kwa madereva juu ya utunzaji wa barabara zetu" alisema Mbarawa.


Mkuu wa Wilaya hiyo Nurdin Babu alitoa ombi kwa wizara hiyo kufunga taa Maalum za barabarani kuanzia mpaka wa Namanga hadi Yalipo Makao Makuu ya wilaya hiyo kutokana na barabara hiyo kuwa kipitio Cha watali kutoka mataifa Mbalimbali.


" Kama mnavyojua shughuli zimefunguka mpakani hapa na watali kutoka nchi jirani ya Kenya wanapita hapa , Tunaomba kwa kuwa tupo mpakani kumsaidia Mh Rais hususani katika kukusanya mapato,TRA katika kituo kimoja cha forodha ilipanga kukusanya sh.bilion 64 lakini wamevuka lengo na kukusanya sh.bilion 89 hadi Sasa,naomba tusaidie tupate taa hizo" alisema Babu.


Naye Mbunge wa jimbo hilo ambae pia ni Naibu Waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa alitoa shukrani kwa Rais Samia kwa kujenga kituo hicho Cha kupimia uzito wa Magari,lakini pia alitoa ombi kwa wizara hiyo kumalizia ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 44 kwa kiwango cha lami.


" Kutoka kata ya kamwanga hadi kata ya Olmolog kwenye kijiji cha Elerai hakuna barabara ya kiwango cha lami na barabara hii ni ya kiuchumi kwa kusafirisha mazao ,imening'inia tuu naomba uimalize kipande hiki" alisema Dkt Kiruswa.


Naye mwakilishi wa wazee wa mila wilayani hapa (Alaigwanani) Thomas Ole Ngulipa alitoa ombi kwa serikali kutoa kipaumbele cha ajira kwa wazawa wa wilaya hiyo hususani kutoka katika kata ya kimokouwa kutokana na wananchi kutoa eneo la ujenzi,hivyo jamii wanufaike na mradi huo.


Mtendaji Mkuu wa wakala wa barabara  nchini (TANROAD)Mhandisi Rogatus Mativila alisema mradi huo umejengwa kwa fedha za ndani hapa nchini Sh.Bilion 14. ,lakini tatizo lililopo kwa sasa ni wafugaji kuingiza mifugo katika eneo la mizani pamoja na uharibifu wa alama za barabarani na thamani kwa  watumiaji wa barabara.


" Mradi hii uliwanufaisha wananchi kwa ajira za kudumu na za muda mfupo,watanzania 270 walipata ajira huku wageni wakiwa 12 pekee lakini pia mamalishe walinufaika kwa kuuza vyakula"alisema Mhandisi Mativila.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela alisema wilaya ya Longido ni wilaya ya kimkakati katika Mkoa wa Arusha kutokana na wilaya hiyo kuwa eneo la Uwekezaji na vyote vinavyofanyoka ikiwemo miradi ya Maendeleo vinaongeza thamani ya Mkoa huo.


Alisema eneo hilo linavivutio vingi vya utali hususani katika barabara ya kilomita 110 kutoka Makao Makuu ya wilaya Hadi kufika katika eneo la ikolojia ya Ziwa Natron Kuna vitalu vingi vya Uwindaji.


" Barabara hii ya kilomita 110 ikijengwa kiwango Cha lami itasaidia kufungua korido ya utali kutokana na barabara hii kuunganisha mapitio ya utali wa Ziwa Natron pamoja na waso huko Ngorongoro" alisema.


Aidha alidai baada ya Rais Samia kufanya ziara nchini Kenya ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara,mpaka wa Namanga kibiashara umefunguka  hivyo wanapambana kuimarisha na kukuza Uchumi wa nchi.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa akizindua Mizani ya Kimokouwa Wilayani Longido akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha pamoja na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Rogatus Mativila pamoja na Naibu Waziri wa Madini DKT Stephen Kiruswa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela 



Waziri wa Ujenzi Prof.Makame Mbarawa akiangalia Utendaji wa Mizani ya Kimokouwa mara baada ya kuizindua Wilayani Longido Mapema Jana 






Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: