Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Shauri Selenda (wenye suti nyeusi) akizungumza baada ya kukagua bidhaa zinazouzwa na mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF, Asha Mwijuma (kushoto) mkoani Pwani leo Juni 15, 2022.
Afisa Mwandamizi wa Uchumi kutoka Benki ya Dunia Michelle Zini ambao ni miongoni wa wafadhili wa TASAF akizungumza wakati akikagua vitenge vinavyouzwa na wanufaika wa TASAF.
Watendaji wa TASAF na wanufaika wakiwa kwenye mkutano.
Mnufaika wa TASAF, Simwana Abdallah akiwa mbele ya nyumba yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Shauri Selenda (mwenye suti nyeusi) akizungumza baada ya kukagua bidhaa zinazotengenezwa na wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF, John  Stephen na kulia ni Mratibu wa Miradi wa TASAF, Janeth Mtelelah
Mnufaika wa TASAF, Simwana Abdallah akizungumzia jinsi TASAF ilivyomnufaisha.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Matimbwa akitoa taarifa ya jinsi wananchi wa kijiji hicho walivyonufaika na TASAF.

 

Na Dotto Mwaibale, Bagamoyo

 

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), umetoa fedha za ruzuku ya uzalishaji kiasi cha Sh.424,596,015.10 kwa walengwa 1,315 katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Shauri Selenda, alisema hayo leo (16/5/2022) baada ya wafadhili kutoka Benki ya Dunia (WB) na ubalozi wa Uswis walipotembelea na kukagua miradi inayoendeshwa na wanufaika wa fedha za ruzuku zilizotolewa na TASAF.

Alisema fedha hizo zimetolewa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu ambapo wanufaika ambao wanaendesha miradi ya kilimo,ufugaji na biashara ndogondogo walipewa fedha kati ya Sh. 100,000 hadi 500,000.

Alisema walengwa 1315 walionufaika na fedha za ruzuku ya uzalishaji ni kati ya 1,468 waliolengwa na kwamba katika awamu ya kwanza walengwa 1003 walipewa ruzuku ya jumla ya Sh. 245,061,048.

Naye Afisa Ufuatiliaji wa Miradi TASAF, Janeth Mtelelah alitoa mchanganuo kuwa wanufaika wa miradi ya kilimo walipewa ruzuku ya asilimia 60 ya kiwango walichoomba, wanaofanya biashara ndogondogo walipewa asilimia 50 wakati asilimia 70 ya ruzuku ilitolewa kwa wanufaika wanaofanya miradi ya ufugaji.

Alisema kuwa utaratibu uliotumika kutoa ruzuku hizo ni kwamba kila mnufaika aliandika andiko lake la mradi na kisha kuomba fedha ambapo alipatiwa kulingana na vigezo vilivyopo.

Aidha, wafadhili hao kutoka Benki ya Dunia na Ubalozi wa Uswis ambao ni Michelle Zini, Stanley Magesa na Paulina Mrosso walitembelea vikundi viwili vya wanufaika katika Kijiji cha Matimbwa ambapo waliridhishwa na jinsi miradi inavyoendeshwa kwa ufanisi mkubwa.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: