TANESCO Mkoa wa Kagera imeanza rasmi kutumia MFUMO wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao, Unaotambulika kama NIKONEKT.

Meneja wa Mkoa Mhandisi Godlove mathayo akiongea Katika Uzinduzi huo, amewahimiza wakazi wa Mkoa wa Kagera kutumia Mfumo huo kufanya maombi ya umeme pamoja na kuwasilisha Taarifa mbalimbali kwani Mfumo huu ni rahisi kutumia kwa Simu Janja/Smart Phone njia ya kupakua App ya NIKONEKT inayopatikana Play store, au kwa Simu ndogo kutumia USSD Code ya *152*00# na kufuata maelekezo.

Watumiaji wa Mfumo huu watapata faida nyingi ikiwemo kuokoa muda na gharama ya nauli kufuata huduma umbali mrefu kwa kuzingatia sasa mteja anaweza kuomba huduma akiwa nyumbani kwake au popote Kwenye mtandao, Pia Mfumo unazuia na kuepusha matukio ya Rushwa na Urasimu.

Aliongeza kwa kusema leo ikiwa siku ya Kwanza ya kutumia mfumo Hadi kufikia Saa 7:00 mchana Tayari Mkoa ulikua umepokea jumla ya maombi Mapya 65.

Tukio hili la uzinduzi wa ufumo wa NIKONEKT uliongozwa na Meneja wa Mkoa Mhandisi Godlove Mathayo pamoja na Afisa uhusiano Mkoa Samuel Mandari, liliambatana na kukata Keki na wateja watano (5) wa awali waliowasilisha Maombi kupitia mfumo ambao walikula pamoja na wafanyakazi wa TANESCO

Imetolewa na:-
OFISI YA UHUSIANO TANESCO KAGERA
Share To:

Post A Comment: