Na John Walter-Simanjiro

Mwenge wa Uhuru upo mkoani Manyara ambapo umeanza mbio zake katika wilaya ya Simanjiro juni 13 ukitokea mkoani Kilimanjaro.

Aidha Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 umesita kufungua,kuweka mawe ya msingi miradi mitatu katika wilaya ya Simanjiro ambayo imekutwa na dosari mbalimbali.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Sahel Geraruma amewataka viongozi kusimamia vyema miradi inayotekelezwa kwa fedha za serikali ili walengwa ambao ni wananchi wanufaike na miradi hiyo kama ilivyokusudiwa.

Moja baada ya kufanya ukaguzi kwenye mradi wa Ujenzi wa darasa moja katika Shule ya Sekondari Terrat iliyojengwa kwa fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19 mwaka 2021/2022 shilingi Milioni 20,0000,000 wamebaini kuwa limejengwa chini ya kiwango.

Pia Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2022 Sahel Geraruma  amelazimika kuwanyang'anya leseni madereva sita wa Kikundi cha Vijana wanaofanya biashara ya usafirishaji  kwa kutumia pikipiki (bodaboda Family) kilichopokea mkopo wa Halmashauri shilingi Milio 14,100,000 kwa kushindwa kujibu maswali yanayohusiana na usalama barabarani na kuwataka kurudi darasani kujifunza na kuelewa alama na ishara barabarani.

Pia Mwenge wa Uhuru uligoma kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa kituo cha Afya kata ya Terrat inayojengwa kwa fedha za tozo kutoka serikali kuu kwa gharama ya shilingi Milioni 500.

Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 katika mkoa wa Manyara zitahitimishwa Juni 19 katika wilaya ya Mbulu.

Share To:

Post A Comment: