Kiongozi wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru Mwaka 2022, Sahili Nyanzabara Geraruma (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja mara baada ya kuwasili wilayani juzi mkoani Manyara kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Miradi ikikaguliwa na kuzinduliwa.
Mmoja wa mradi wa maji wa RUWASA uliokaguliwa.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakipitia michoro mbalimbali wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo.
Mradi wa majiukiwa umekamilika.
Mwenye wa Uhuru ulivyo pokelewa wilayani humo.
Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yakiendelea.
Vijana wa Skauti wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Mwenge waUhuru ukipokelewa.
Shamra shamra za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru zikiendelea.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na lasama wa wilaya hiyo wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
 

 

Na Dotto Mwaibale, Hanang'

 

KIONGOZI wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru Mwaka 2022, Sahili Nyanzabara Geraruma ameweka Jiwe la Msingi kwenye miradi na kufanya ukaguzi wa miradi hiyo yenye gharama ya zaidi ya Sh. Bilioni moja..

Akizunguza juzi Juni 17,2022 wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo Mkuu wa Wilaya Hanang' Janeth Mayanja aliitaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Maji Gidangu - Gidahababieg wenye thamani ya Tsh 120m, Mradi wa ujenzi wa madarasa manne Nangwa Sekondar wenyei  thamani ya Sh 84 Milioni, mradi wa ujenzi wa jengo la dharura Hospitali ya Tumaini wenye thamani ya Sh 300 Milioni, ujenzi wa madarasa mawili Ganana Sekondari  wenye thamani ya Sh 38 Milioni, mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Barabara ya Mkapa wenye thamani ya Sh. 499 Milioni na mradi wa kikundi cha Vijana  Dream Studio and Stationery wenye thamani ya Sh 15 Milioni wa Kata ya Katesh.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Geraruma ameridhika na utekelezwaji wa miradi yote sita aliyoitembelea na kuikagua ambapo aliithibitisha na kutoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja na Taasisi zote za Serikali zilizopo wilayani humo kama Ruwasa, Tarura, Halmashauri na wananchi kwa kutekeleza miradi hiyo kwa viwango.

Geraruma alitumia nafasi hiyo kuwahimiza  watumishi wa Umma kusimamia miradi yote inayotekelezwa kwa wakati na kuzingatia miongozo.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: