Na John Walter-Manyara


Mbio za Mwenge wa Uhuru Katika mkoa wa Manyara utakimbizwa katika Halmashauri tano za mkoa huo na kutembelea miradi 39 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 23.2.


Miradi 17 yenye thamani ya shilingi Bilioni 20.7 itawekwa mawe ya msingi, Bilioni 1.6 itafunguliwa huku mingine  Tisa yenye thamani ya shilingi milioni 843.7 ikitembelewa.


Aidha katika mkoa wa Manyara Mwenge utakimbizwa Katika Mamlaka za Serikali za mitaa Saba ambazo ni Simanjiro,Kiteto,Babati mji,Babati wilaya,Hanang,Mbulu wilaya na Mbulu mji kwa mzunguko wa kilometa.


Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere ameahidi kusimamia vyema Mwenge huo Kipindi chote utakapokuwa ndani ya Manyara. 

  

Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 leo Juni 13 umeanza kukimbizwa Katika mkoa wa Manyara ukitokea  mkoa wa Kilimanjaro na kilele chake ni Juni 19.


Akikabidhi Mwenge huo kwa mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai amesema katika mkoa wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Sahil Geraruma amekagua na kufungua miradi 38 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 13.


Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 zitafikia kilele chake Oktoba 14, 2022 mkoani Kagera zenye kauli mbiu Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo: Shiriki kuhesabiwa, tuyafikie Maendeleo ya Taifa.

Share To:

Post A Comment: