Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya amevipongeza Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kutoa maarifa  mbadala kwa changamoto zinazoikabili jamii. Hii inatoa hamasa kwa sababu wanaungana na sera za nchi katika kuongeza fursa za kupata ajira.


“Mafunzo ya Elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi Stadi yanagusa eneo muhimu sana la vijana, vijana wengi wamepata elimu hii kwa mafunzo ya muda mfupi miezi mitatu, miezi sita, miaka mitatu ambayo yanawawezesha kupata ujuzi mbalimbali katika utendaji kazi  pamoja na kutoa vyeti.”


 Amesema hayo alipotembelea Maonesho ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi yanayofanyika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma ambayo yamesaidia  kutoa maarifa kwa wananchi kujua fursa za ajira zilizopo katika maeneo yao, lakini pia kusaidia wataalamu wetu kuwa na maarifa yanayoendana na soko la ajira linalohitajika katika Nchi yetu


Naibu katibu mkuu Mmuya ametoa rai kwa wanavyuo na  wakufunzi kuendelea kuangalia mahitaji ya jamii ili waweze kuandaa mafunzo ya muda mfupi  ili kuweza kuwapatia wananchi ujuzi unaotakiwa utakaosaidia kuzalisha ajira nyingi.


Naye Mkurugenzi mtendaji wa mitala na upimaji Dr. Annastelllah Sigweyo amesema baraza inaangalia program zinazoanzisha zainaendana na uhitaji wa jamii baada ya kufanya utafiti wa eneo husika na kwa kuzingatia ushauri wa wadau.


tunaangalia uwezo wa chuo kinachotaka kutoa program kama kina uwezo wa kutoa ujuzi husika kwa kuangalia uwezo wa walimu kitaaluma katika kutoa ujuzi, ndipo tunapopitisha mtaala kwa ajili ya chuo husika.


 


 



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu,Bwn. Kaspar Mmuya akizungumza katika moja ya banda baada ya kutembelea maonesho ya vyuo vya ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayofanyika uwanja wa jamhuri Mjini Dodoma.




Mhadhiri wa chuo cha Afya Mvumi John Bwn. John Mpiluka (kulia) akimuelezea Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya shughuli zinazofanywa na chuo cha afya Mvumi katika banda lao la maonesho ya vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.




Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu,Bwn. Kaspar Mmuya akiwa katika banda la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalumu linalosimamia vyuo vilivyo chini ya wizara hiyo katika maonesho ya Vyuo vya elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.





Dkt. Annastellah Sigweyo (katikati) akieleza shughuli zinazofanywa na Baraza la Taifa la Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) katika maonesho ya Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: