Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga Burhan Yakub akiuliza jambo wakati wa semina hiyo |
Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV na Radio One Mkoa wa Tanga Wiliam Mngazija akiuliza swali katika semina hiyo |
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
MAMLAKA
ya Hifadhi ya Ngorogoro (NCAA) imeanza mkakati kabambe kwa kuleta
Mapinduzi Makubwa ya kiutalii katika Mkoa wa Tanga kupitia Mapango ya
Amboni baada ya kueleza dhamira yao ya kutaka kuunganisha utalii
unaofanyika kwenye mapango ya Amboni na Visiwani Zanzibar.
Mkakati
huo ulitangazwa na Mkuu wa Kanda wa Hifadhi ya Mapango ya Amboni
Mecksadeck Mwambungu wakati wa Semina kwa waandishi wa habari
iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mwambunhu
ambaye pia ni Afisa Malikale Amboni kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro alisema mkakati huo unakwenda sambamba na kuhakikisha
wanafanikisha upatikanaji wa boti ya watalii wanaotoka zanzibar
iliwaweze kukaa amboni kwa muda kidogo.
“Kwa
kweli mkakati wetu ni kuhakikisha tunaunganisha utalii unaofanywa
mapango hayo na Visiwani Zanzibar na tunakusudia kuhakikisha
tunafanikisha upatikanaji wa boti kwa lengo la kuwawezesha wakija kwenye
mapango hayo wanakaa muda mrefu”Alisema
Bw.
Mwambungu ameongeza kuwa NCAA wanamkakati wa kuanzisha utalii wa
Boarder(mpakani) kwani kuna watu wanatamani kufika Kenya na hawajui
watafikaje na kutoka Horohoro mpaka Amboni ni Kilomita 60 hivyo
wanataka kuweka mpango wa kuweka utaratibu mzuri wa kuwawezesha kufika
na kufurahia utalii.
“Lakini
tatu tunataka kuangalia vivutio vya vilivyopo jirani na Tanga tuweze
kuviinua vikiwemo Marine Park na eneo la Maji Moto tunaamini tukiviinu
vizuri vitaleta tija kubwa”Alisema
Hata
hivyo alisema suala lingine ambalo wanalifikiria ni kutaka kuhakikisha
kwamba wanaongeza idadi ya watalii kwenye eneo la Mapango ya Amboni na
wanaamini kutokana na mikakati walioweka utafanikiwa.
“Kwa
sasa tunapokea watalii karibia 1000 mpaka 2000 wengi ni wenyeji na
wageni ni wachache sana hivyo tunaamini kutokana na maboresho
yaliyofanyika ya miundombinu itakuwa ni fursa nzuri kwao kuweza kuongeza
idadi hiyo “Alisema
Hata
hivyo alisema kwamba mpango wao waliokuwa nao kwa sasa ni kuanzisha
ulipaji kwa njia ya mtandao na mahitaji muhimu kwa watalii ambapo
wanaamini utakuwa na manufaa makubwa.
Awali
akizungumza wakati wa semina hiyo Kaimu Meneja Uhusiano wa Umma wa NCAA, Joyce Mgaya alisema eneo la Mapango ya Amboni limekuwa na
simulizi nzuri na ya kuvutia kutokana na kwamba ndani ya mapango kuna
eneo ambalo watu wanafanya ibada wa imani tatu tofauti kwa wakati mmoja
na wanaweza kuabudu na kuamini sawa kwamba wakienda hapo wanafanya ibada
na kuaminiana
“Hivi
sasa kuna utandazawazi mkubwa baadhi tunapoteza hamasa ya kupenda
simulizi zetu au kupenda vya kwetu na badala yake tunathamini simulizi
za nje ..nadhani kwenye mapango kuna mtu anasafiri kutoka nje ya nchi
anakuja kufanya tambiko na kuondoka”Alisema
Hata
hivyo alisema kwamba wanafikiria kuweka kitanda kwenye mapango ili watu
wanaokwenda kutalii eneo hilo waweze kupata eneo la kupumzika usiku na
kuweza kusikilizia usiku kunakuwaje.
Post A Comment: