Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro leo Tarehe 15/06/2022 amemshukuru Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia maafisa ugani wote 32 kupatiwa pikipiki mpya za kisasa katika wilaya ya ikungi 


Dc Muro amesema hayo wakati wa zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa maafisa ugani ambapo amesema  lengo la pikipiki hizo ni Kuwawezesha maafisa ugani wa kilimo kutoa huduma za ugani kwa wakati kwa wakulima wa vijiji vyote 101 katika wilaya ya ikungi.


Awali akitoa taarifa ya pikipiki hizo Afisa kilimo na umwagiliaji wilaya ya ikungi ndugu Gurisha Msemo amesema Pikikipi hizo zitasaidia kurahisisha huduma za ugani kwa wakulima pamoja na Kuongeza uzalishaji kwa tija ikiwemo kukusanya takwimu za wakulima kwa wakati pamoja na Kupunguza gharama za usimamizi na ufatilijiaji kwakuwa watakuwa na vitendea kazi hawatakodi tena usafiri
Share To:

Post A Comment: