Na,Jusline Marco;Arusha


Naibu Waziri,Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Mwanaidi Ali Khamisi amewataka wadau wa mashirika binafisi kushirikiana na serikali katika kuhamasisha sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 mwezi Agost mwaka huu.

Mhe.Mwanaidi ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa ushirikishaji wa wadau wa ukanda wa Kaskazini kuhusu maendeleo ya mkakati wa kitaifa wa Uendelevu wa NGOs wa kukusanya maoni uliofanyika jijini Arusha .

Aidha Mhe.Mwanaidi amesema wizara yake itaendelea kudumisha ushirikiano kwa ajili ya kuyajengea uwezo mashirika hayo ili kupunguza utegemezi na kuwa endelevu kwa shughuli wanazozifanya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali,Musa Khamis kwa niaba ya msajili qa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini,amesema lengo la mkutano huo ni ukusanyaji wa maoni kwa wadau wa NGOs kueleza uhitaji wao ili kuweza kuondokana na utegemezi huo.

Naye Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Arusha Bi.Blandina Nkini ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo ambayo yametolewa.


Hata hivyo mkutano huo ni muendelezo wa vikao ambavyo vimeshafanyika katika mikoa mingine ikiwemo Mkoa wa Mwanza, Pwani ,Kilimanjaro,Manyara ,Tanga na Arusha.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: