Na;Jusline Marco;Arusha


Waziri wa Katiba na sheria Dkt.Damas Ndumbaro ameipongeza ofisi ya wakili mkuu wa serikali kwa kuokoa fedha zaidi ya trilioni kumi na kurejesha mashamba 103 serikalini.


Akifunga mafunzo kwa mawakili 600 wa taasisi za serikali yaliyofanyika jijini Arusha ya kuwajengea uwezo mawakili wa serikali ambapo amewataka kuongeza bidii na kuzingatia miiko ya kazi zao na kutobweteka kutokana utendaji mzuri ulioleta  maafanikio makubwa tangu kuanzisha kwa ofisi ya wakili mkuu wa serikali.


Dkt.Ndumbaro amesema mafunzo waliyoyapata yakawe chachu ya kuwafanya waendelee kufanya vizuri zaidi kati utendaji kazi wao.


“Ofisi hii ni moja kati ya ofisi changa katika wizara ya Katiba na sheria lakini ni taasisi ambayo tangu kuanzisha kwake imeifanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu, utendaji wa kazi wa ofisi hii unaonekana bayana kwa kumeoko fedha nyingi na mali za serikali,”Alisema Dkt.Ndumbaro


Aidha Dkt.Ndumbaro amesema kama wizara ya Katiba na sheria itaendelea kutoa ushirikiano kila itakapohitajika ambapo ni matarajio yao kama wizara mafunzo hayo yataenda kuwa chachu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali ya kisheria ambayo inaikabili serikali na taasisi zake pamoja na kwenda kupunguza mashauri kwenye mahakama na maeneo mengine ambayo serikali inakabiliana nayo.


Sambamba na hayo amewataka mawakili hao kuziheshimu sheria pamoja na kupambana na Rushwa kwakuwa wao wanafanyakazi katika mfumo wa kutoa haki hivyo Rushwa ni adui wa haki hivyo ni lazima waepuke jambo hilo.


Wakili Mkuu wa serikali Gabriel Malata  amesema kuwa majukumu ya ofisi ya wakili mkuu wa serikali ni kuratibu, kusimamia  na kuendesha mashauri yote yanayohusika katika mashirika na kampuni ambazo serikali ni mwahisa muhimu.


Malata amesema Ofisi ya wakili Mkuu wa serikali ni kiungo kati ya wizara ya Katiba na sheria na miimili yote mitatu ambapo kupitia mawakili hao wameendelea kuhakikisha wanaendesha na kunapunguza mashauri yote yaliyopo mahakamani na tunapunguza idadi ya migogoro na mashauri.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: