Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro leo Tarehe 26/05/2022 ameanza kazi ya utatuzi wa mgogoro wa Ardhi baina ya kata mbili za Dung'unyi na Puma katika eneo la vijiji vya Wibia na Dung'unyi katika mbuga ya Njori 


Dc Muro akiambatana na kamati ya usalama ya wilaya amekutana na na viongozi wa pande zote mbili pamoja na familia za wananchi wanaovutana katika eneo hilo hatua ambayo imeanza kuhatarisha amani na usalama wa mbuga hiyo inayotumiwa kwa kilimo na mifugo


Wakitoa taarifa za awali mwenyekiti wa kijiji cha Wibia Daniel Benedict Amasi na Alex Mateo Jingu wa kijiji cha Dung'unyi wamesema mgogoro huo ambao umeanzia katika familia mbili umeanza kuchukua sura ya mgogoro wa vijiji kutokana na utata wa mipaka inayotengeneza vijiji vyao


Katika hatua ya awali ya usikilizaji wa mgogoro huo ofisi ya mkuu wa wilaya imeanza kusikiliza pande zote za uongozi wa vijiji, familia zinazopingana uku ikizingatia maelekezo ya mkuu wa wilaya aliekuwepo wakati wa mapigano katika eneo hilo Mhe. Miraji Mtaturu pamoja na kuzingatia hukumu za mabaraza ya ardhi zilizopo


Share To:

Post A Comment: