Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud akitoa hotuba yake ya ufunguzi.
Prof. Gerald Misinzo akitoa maelezo kwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud alipotembelea banda la SUA.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda akitoa maelezo kwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud kuhusu panya wanavyoweza kutambua makohozi yenye TB sambamba na utambuzi wa mabomu.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda akifafanua jambo kwa Mkurugenzi  Mkuu wa TIRDO Prof. Madundo Mtambo alipotembeea banda la SUA kwenye maonesho ya MAKISATU jijini Dodoma.
Maelezo yakitolewa katika wiki ya kitaifa ya Ubunifu kwa mwaka 2022 jijini Dodoma.
Wanafunzi wakiwa nje ya banda la SUA.
Mmoja wa wanafunzi akipata maelezo alipotembelea banda la SUA.
Maelekezo yakitolewa kwa wanafunzi.
Wanafunzi wakipata maelekezo walipotembelea banda la SUA
Wanafunzi wakipata maelekezo walipotembelea banda la SUA
Miche ya mahembe ikioneshwa.
 


Na Calvin Gwabara, Dodoma


SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimedhamiria kujenga uwezo wa ndani wa kwa kuendelea kuwekeza katika rasilimali watu,miundombinu na vifaa vya kisasa vya utafiti na ubunifu pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya taasisi za sayansi na teknolojia na sekta ya viwanda ili kuchochea ubunifu na uvumbuzi nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akizindua wiki ya kitaifa ya Ubunifu kwa mwaka 2022 Jijini Dodoma.

“Matunda ya jitihada hizo za Serikali katika utekelezaji wa malengo hayo na hatua zinazochukuliwa yote yanabainika kupitia mashindano ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na ubunifu ambapo jumla ya wabunifu 2,785 wameweza kuibuliwa mwaka hu una miongoni mwao wale walio mahiri zaidi ya 200 wameendelezwa na Serikali”alieleza Mhe. Masoud.

Amessitiza kuwa lengo kuu la Serikali ni kuwa Wabunifu na teknolojia zao walizozalisha ziweze kufikia hatua ya kupelekwa sokoni na kutumika na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuchangia pato la taifa.

Mhe. Masoud amemesema katika kuhakikisha unifini na elimu ya sayansi na teknolojia inawekezwa kwa vijana ili kupata wataalamu wa fani mbalimbali kwa upande wa Zanzibar tayari wameshaanzisha mradi wa kujenga vituo 22 vya ubunifu wa sayansi unguja na pemba ambavyo vimeanza kutumika mradi wenye thamani ya USD Milioni 35 zikiwa ni mkopo kutoka banki ya dunia.

Amesema Serikali itaendelea kuwekeza kuibua,kutambua na kuendeeza ununifu na teknolojia hapa nchini na kuhamasisha matumizi yake katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi katika masuala ya kijamii na kiuchumi.

Awali akizungumza kabl ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi maonesho hayo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof. Adolf Mkenda amesema maadhimisho hayo ya MAKISATU yanayofanyika kwenye mikoa 16 ya Tanzania  ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya awamu ya sita ya kuongeza hamasa ya matumizi ya sayansi teknolojia na ubunifu kama nyenzo ya kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na jamii.

“Wiki ya ubunifu ya kitaifa inahusisha majukwaa,majadiliano kuhusu maendeleo ya sayansi teknolojia na ubunifu nchini,mafunzo na semina kwa wabunifu ikiwemo elimu ya ujasiliamali aidha mijadala hiyo inawahusisha Watafiti,Wavumbuzi na wabunifu na wadau mbalimbali wa ubunifu na serikali katika kuweka mikakati mbalimbali ya pamoja katika kuhamasisha matumizi ya teknolojia na ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii”alieleza Prof. Mkenda.

Mhe. Mkenda amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya mashindano hayo ya MAKISATU jumla ya wabunifu 1785 wameibuliwa na kutambuliwa na wizara kwa kushirikiana na wadau wengine na kwamba wabunifu mahiri 200 wanaendelezwa na wizara kupitia tume ya taifa ya sayansi na teknolojia COSTECH ili ubunifu wao ufikie hatua ya kuwa bidhaa na kuingia sokoni na kuongeza fursa za ajira na kipato cha vijana nchini na tayari bunifu 26 zimeingia sokoni.

Amesema katika mashindano hayo ya mwaka huu 2022 jumla ya wabunifu 86 wamepatikana kutoka katika makundi yote nchi nzima  ili kushindanishwa na mwisho siku ya kilele wapatatokana washindi ambao watatunukiwa zawadi na bunifu zao kuendelezwa na Serikali kupitia COSTECH.

Akitoa neno la shukrani Mwakilishi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambao ni ndio wafadhili wakuu wa MAKISATU Bi. Christine Musis amesema wataendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kujenga utamaduni wa Ubunivu na uvumbuzi nchini..

“Niko hapa kama mdau mkubwa wa serikali katika kusaidia kuchochea ubunifu kwa vijana wa kitanzania na kuwapa kianzio cha masaada wanaohitaji kupiga hatua kutoka mawazo,sampuli kifani hadi kufikia hatua ya kufika sokoni ili wawe injini ya ukuaji na maendeleo nchini Tanzania”alisisitiza Bi.Musis.

Awali kabla ya kufungua wiki hiyo ya kitaifa ya Ubunifu Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud na viongozi wengine wa Wizara na serikali walitembelea mabanda mbalimbali yanayoonyesha bunifu na teknolojia mbalimbali ikiwemo banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na kuvutiwa na maelezo ya namna panya wanavyoweza kutambua makohozi na mtu mwenye TB na kugundua mabomu maelezo yaliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda na baadae kupata maelezo kutoka kwa Prof. Gerald Misinzo  na  kuona namna Gari ambalo ni maabara inayotembea ya SUA ainavyofanya kazi.


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: