Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amechangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya ofisi ya BAKWATA Mkoa wa Mbeya.


Mwaka jana katika Baraza kama hili Mahundi alichangia pia ujenzi wa ofisi hiyo akiwakiwakilishwa na Dkt Tulia Ackson.


Mahundi ameungana na Waislam wa Mkoa wa Mbeya katika Baraza la Eid lililofanyika Uwanja wa Sokoine Mbeya.


Aidha Mahundi amewasilisha salam za Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson ambaye ni Mbunge wa Mbeya mjini.


Share To:

Post A Comment: