Na Ahmed Mahmoud


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana anatarajiwa kufungua maonyesho ya kimataifa ya utalii ya Karibu Killfair yatakayofanyika Jijini Arusha kuanzia June 3 hadi 5  2022.

Aidha  Zaidi ya waonyeshaji 350 kutoka nchi 12 duniani, wanatarajiwa kushiriki maonyesho ya Kimataifa ya utalii ya  Karibu  Kilifair,ambayo yatafanyika kwa mara ya kwanza baada ya kusitishwa kwa miaka miwili kutokana na  janga la Uviko-19,yanategemea kuvutia washiriki kutoka Afrika Mashariki na wanunuaji kutoka masoko ya kimataifa.

Akizungumzia maonyesho hayo ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Promotion,ambao ndiyo waandaaji wa maonyesho hayo,Dominic Shoo,amesema maonyesho yanayotarajiwa kufanyika Juni 3 hadi 5,2022 yatafunguliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Pindi Chana.

Amesema kuwa mwaka huu maonyesho hayo yatakutanisha waonyeshaji zaidi ya 350 kutoka nchi 12,wanunuzi zaidi ya 400 kutoka nchi 38 ambapo wanatarajia kuwa na wahudhuriaji 7,000 katika siku zote tatu.

Alisema maonyesho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya Magereza,yamelenga kujenga biashara na kufanya wadau wa utalii kukutana baada ya changamoto ya muda mrefu ya Uviko-19.

“Tukio hulu limevuta hisia kubwa kutoka kwa wadau jambo ambalo linaonyesha kuwa watu wana hamu kubwa ya kukuza biashara zao na tunatarajia yatakuwa ya namna ya kipekee,”amesema

Kwa upande wake Meneja wa NMB,Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper,amesema wameshiriki kwenye maonyesho hayo kwa sababu wanaamini utalii ni sehemu kubwa ya uchumi katika kanda hiyo na taifa kwa ujumla.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa sekta ya utalii nchini,wameamua kuwa na mahusiano na waandaaji wa maonyesho hayo ambapo wamechangia Sh milioni 59.

“Tunahitaji kukuza sekta hii ya utalii kwani sekta hii ikikua na kustawi itachangia kuongeza mapato,na ndiyo maana kama wadau wa utalii tumechangia Sh milioni 59 ili maonyesho yaweze kufanikiwa,”amesema Dismas
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: