Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro leo tarehe 23/05/2022 amehitimisha mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la KIWOHEDE Mama Justa Mwaituka ambae kwa pamoja wamekubaliana kuanza ujenzi wa jengo la kisasa la MKONO SHUFAA jengo lenye thamani ya shilingi Milioni 117 

Jengo hili litajengwa wakati wowote kuanzia sasa katika hospitali ya Wilaya ya Ikung kwa ajili ya kuratibu na kusimamia shughuli za upingaji wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike na kiume na wanawake katika Wilaya ya Ikungi ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wilaya zinakomesha matukio na vitendo vya ukatili wa kijinsi kwa watoto na wanawake 

Dc Muro amesema wao kama wiliaya wameona waweke utaratibu utakaotuwezesha kupambana na matukio yanayozidi kuongezeka ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wetu na wanawake kwa kujenga mifumo imara ya kuratibu na kushughulikia changamoto hii ambayo imeendelea kuongezeka katika Wilaya

Dc Muro ameongeza kuwa Maono ya wilaya ni kuona wanabadili 

 mwelekeo ambao hautamtazama mtoto wa kike peke yake bali utawatazama watoto wote kama wahanga wakuu wa matukio ya ubakwaji, ulawiti, utumikishwaji wa kazi za majumbani na vitendo vingine vya ukatili ikiwemo watoto wanaozunguka na kuombaomba mitaani 

Kwa upande wakw Mkurugenzi wa KIWOHEDE Mama Mwaituka amesema wameridhishwa na jinsi wilaya inapambana katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsi na kwa kipindi chote walichofanya kazi ikungi wameridhishwa na ushirikiano na namna halmashauri inatekeleza maelekezo ya kutokomeza vitendo hivyo japo bado jitihada zaidi zinahitajika katika kumaliza tatizo hilo 

Nichukue fursa hii kuwashukuru wenzetu wa KIWOHEDE kwa kuendelea kufanya kazi na sisi, nimshukuru sana Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi na team yake kwa kuratibu jambo hili kwa haraka na sasa tunakwenda kuongeza thamani katika kuwalinda watoto na wanawake katika Wilaya kwa mkakati na ubunifu mpya amehitimisha Dc Muro 

 *Tazama picha za matukio* πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

 *Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ikung*IKUNGI NA KIWOHEDE KUANZA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA MILIONI 117* 

 Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ikungi

Share To:

Post A Comment: