Na Joel Maduka Geita…


Mgodi wa dhahabu wa Geita GGML wametoa vyakula mbali mbali, ukiwemo mchele Kilo 500 pamoja na mafuta Lita 100 na Ng’ombe wawili, lengo likiwa ni kushiriki na watu wenye uwitaji katika siku kuu ya Eid.

Hatua hiyo ya mgodi imetokana na mahusiano mema ambayo imeendelea kuwa nayo juu ya waumini wa dini hiyo.


Akikabidhi msaada huo Afisa Uhusiano wa mgodi wa GGML  Mussa Shonashu,amesema wameamua kufanya hivyo ikiwa kama sehemu ya kutoa sadaka kwa watu wasio jiweza hili nao waweze kusherekea siku kuu hii ya EID.


“ msaada huu kutokana na kuwa na ushirikiano mzuri bahina yetu na waumini wa dini ya kiislamu tunajua sio kingi tulichotoa lakini imani yetu kitasaidia walau baadhi ya watu wenye uhitaji” Mussa Shonashu Afisa Uhusiano wa mgodi wa GGML.


Kwa upande wake  Shekhe Mkuu wa mkoa wa Geita.Alhadi Yusufu Kabaju amehushukuru mgodi wa GGM kutokana na namna ambavyo umeendelea kuwa karibu na jamii ambayo inauzunguka.


“Kwa niaba ya waislamu mkoa wa Geita tunatoa shukrani kwa mgodi wa GGML kwa kutoa msaada huu sisi tutawagawia watu wenye uwitaji wakiwemo wajane, yatima na familia ambazo hazina uwezo” Alhadi Yusuf Kabaju Shekhe mkuu wa mkoa wa Geita.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: