Na,Jusline Marco;Arusha


Taasisi ya fedha Benki ya CRDB imejipanga kuangalia fursa mpya na kuhakikisha wanaendelea kutoa bidhaa zinazohitajika na wateja.


Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Abdulmajid Nsekela katika Mkutano wa 27 wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika jijini Arusha,amesema kuwa muda uliobaki wa mwaka 2022 Benki hiyo itahakikisha huduma zinazotolewa zinamfikia kila mteja kwa kutoa bidhaa zinazohitajika.


Nsekela alisema kama benki itaendelea kuhakikisha wanahudumia wateja kwa haraka nchini  kupitia Benki fasta pamoja na kuendelea kuwa makini na athari zinazoweza kujitokeza kwa kuweka miundo mizuri ya viashiria vya majanga.


“Tumekuwa na mahusiano ya karibu na wajasiriamali na wafanyabiashara hasa akina mama kwa kuanzisha huduma mahususi kwaajili yao pamoja na asilimia 93 ya huduma zetu kufanyika nje ya matawi  kutokana na uwezeshwaji mkubwa wa teknolojia,” Alisema Nsekela.



Kwa upande  wake Mkurugenzi wa fedha katika Benki hiyo Fredrick Nshekenabo ameleza kuwa mafanikio wanayoyapata yamechangiwa na mapato yasiyokuwa na riba na kukuza midhania ya Benki inayotokana na uendelezaji wa mkakati wa kudhibiti gharama za uendeshaji kutoka asilimia 61 hadi kufikia asilimia 55.


Amefafanua kuwa mikopo yao imeendelea kukua kutoka asilimia 59 kwa wateja wadogo na asilimia 40.8  kwa wateja wakubwa sawa na asilimia 28 ambapo hadi kufunga mwaka mikopo chechefu ilishuka na kufikia asilimia 3.3  huku kiasi cha fedha kilichopo kama mtaji kikiwa ni trilioni 9.4.


Naye Mkurugenzi mstaafu wa CRDB Dkt.Charles Kimei katika Mkutano huo  amewapongeza viongozi wa benki hiyo kwa kupata faida kubwa ya asilimia 36 pamoja na uwepo wa COVID- 19 ambapo ameshauri benki hiyo kuhusiana na kasi ya ukuaji, kuwa makini kwani ukuaji mkubwa unaogopesha.


“Gawiwo tunalolipata ni zuri na kila mwanahisa anatamani kupata faida kubwa lakini tuweke usawa tusitake kupata faida kubwa, tuweke tozo ambazo zitakuwa na usawa,”Alisema .

Share To:

Post A Comment: