Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu akitoa salamu za benki hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) yaliyoambatana na zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wakubwa wa maadhimisho hayo. Wanaomsikiliza meza kuu ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo (katikati) na Rais wa TRCS, David Kihenzile (Mb)


Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Dodoma Bw Jalala Kizigo akishiriki zoezi la upandaji wa miti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) yaliyoambatana na zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wakubwa wa maadhimisho hayo.Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo (katikati).


Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Dodoma wakiongozwa na Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Dodoma Bw Jalala Kizigo (wa pili kulia) wakishiriki zoezi la upandaji wa miti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) yaliyoambatana na zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wakubwa wa maadhimisho hayo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo (katikati) na Rais wa TRCS, David Kihenzile (Mb) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu (Kulia waliosimama) na Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Dodoma Bw Jalala Kizigo (Kushoto waliosimama) wakati wa kilele cha maadhimisho hayo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo (katikati) na Rais wa TRCS, David Kihenzile (Mb) wakiongoza maandamano ya wadau mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) yaliyoambatana na zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki.

...........................................

Benki ya Exim Tanzania imeahidi kushirikiana zaidi na wadau mbalimbali sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kushiriki kikamilifu katika kuunga mkono jitihada za utunzaji mazingira hususani kwa upandaji wa miti.

Ahadi ya benki hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) yaliyoambatana na zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo yaliyoongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo, Bw Kafu alisema kupitia Program za benki hiyo zijulikanayo kama ‘Exim Go Green Initiative’ na ‘Exim Cares’ benki hiyo imekuwa ikijihusisha na mikakati mbalimbali ya kijamii ikiwemo uchangiaji damu pamoja na utunzaji mazingira kupitia matawi yake yaliyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

“Kwa upande wa ukanda huu wa kati, jiji hili la Dodoma limebahatika kuwa chaguo la Benki ya Exim katika kuendesha Programu hii. Ni Kipindi kama hiki mnamo mwaka jana, tukiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Pinda tuliweza kushirikiana na wadau wengine mkoani hapa katika kupanda takribani miti 10,000 katika kata ya Zuzu iliyopo hapa jijini Dodoma.’’ Alisema Kafu.

Licha ya kushiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji miti, benki hiyo pia ilichangia fedha kiasi cha Sh mil 15 kwa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) ili kufanikisha zoezi hilo la upandaji miti.

Alisema taasisi ya kifedha nchini ikiwemo benki hiyo zimekuwa zikiguswa na athari za kiuchumi zinazotokana na kuzorota kwa sekta za uzalishaji ikiwemo kilimo kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na hiyo imekuwa moja ya sababu kubwa zinazosababisha taasisi hiyo kushiriki mstari wa mbele katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kutunza mazingira ikiwemo upandaji miti.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Waziri Jafo pamoja na kuipongeza benki hiyo pamoja na wadau wengine kwa kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira hapa nchini, aliwataka Watanzania kuungana kwa pamoja katika kujitolea utoaji wa huduma za jamii ikiwemo ushiriki wa uokoaji nyakati za majanga pamoja na ushiriki wa utunzaji wa mazingira kwa upandaji wa miti.

"Na hii ndio sababu nawapongeza TRCS kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa jitihada hizi muhimu na za kizalendo. Ninaomba jitihada hizi ziendelee katika kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotokea,’’ alisema.

Awali akizungumza kwenye maadhimisho hayo Rais wa TRCS, David Kihenzile (Mb) aliiomba serikali na wadau mbalimbali nchini kuendelea kuunga mkono jitihada za Shirika hilo kwa kuwa zinalenga kuisaidia jamii moja kwa moja katika masuala mbalimbali ikiwemo majanga na dharula.

“Ndio maana tumeguswa sana na uungwaji mkono tulioupata kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Exim kwa kuwa msaada wao umetuwezesha kufanikisha zoezi hili muhimu la upandaji miti pamoja na zoezi la uchangiaji damu…tunawashukuru sana tunaomba na wengine waige mfano huo kwa kuwa bado tunahitaji sana uungwaji mkono,’’ alisema Kihenzile.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: