Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ortamisemi Mhe. Innocent Bashungwa ameahidi kushughulikia upungufu wa maofisa habari na mawasiliano katika halmashauri 85 nchini ambazo hazina maofisa hao.


Hayo ameyasema leo Ijumaa Mei 13, 2022 wakati wa kikao cha maofisa habari, mawasiliano na uhusiano Serikalini kilichofanyika kwa siku tano jijini Tanga.


Mhe. Bashungwa amesema katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara mikoa, minne haina maofisa habari na mawasiliano  na katika halmashauri 184 halmashauri 85 hazina maofisa hao ambao amesisitiza kuwa ndio mdomo wa Serikali.


“Hili jambo la kutokuwa na maofisa habari kwangu ni kubwa na la muhimu nipambana nalo kuhakikisha tunakuwa na maafisa habari katika halmashauri 85  ambazo hazina.


“Nitashirikiana na pacha wangu Mhe. Nape na Mhe. Jenista Mhagama kuhakikisha kuwa suala hili tunalifanyia kazi na kulikamilisha,” amesema.


Awali, Katibu Mkuu Wizara Ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jimmy Yonazi alimuomba Waziri Bashungwa kuwasaidia kushughulikia  changamoto  hiyo ya kukosekana kwa maafisa habari katika baadhi ya halmashauri na mikoa nchini.


"Tunaomba utusaidie halmashauri zote na zile Taasisi zilizopo katika ofisi Yako zinapata Maafisa habari," amesema Dk Yonazi.

Hata hivyo, kati ya halmashauri 184 ni halmashauri 99 tu ndo zina maafisa Habari na kati ya mikoa 26 ni mikoa 22 pekee ambayo inamaafisa habari

Share To:

Post A Comment: