Na,Jusline Marvo;Arusha

Kamati ya malaigwanani na viongozi wa kimila na madiwani imekutana jijini Arusha kuhitimisha ripoti ya mapendekezo ya wananchi kuhusu namna bora ya uhifadhi katika tarafa za Loliondo,Ngorongoro na Sale Wilayani Ngorongoro.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Laigwanani wa Mila ya Wamaasai,Metui Ole Shaudo akizungumza jijiji Arusha na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi Ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu Mei 25 mwaka huu,amesema mtazamo wao ni kutegemea ripoti hiyo kusomwa na kisha kuitwa kwa pamoja na kuridhiana ili kuweza kupata suluhu kutoka serikalini.

"Tunatumaini mapendekezo haya serikali itatoa matokeo chanya kwa ajili ya ustawi wa wananchi wa Ngorongorona utaleta suluhu katika utatuzi wa migogoro ya ardhi katika eneo lenye kilometa za mraba 1500 bila kuathiri pande zote mbili,"alisema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafugaji na Diwani wa kata ya Nainokanoka,Edward Maura amesema wanaishukuru serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu kwa kutoa fursa kwa wananchi wa wilaya ya Ngorongoro kuunda kamati na kuandika mapendekezo ya jamii juu ya mwenendo wa changamoto zilizopo wilayani hapo.

"Na kupitia kamati iliyokuwa na wajumbe wa pande zote katika jamii tumeikamilisha hiyo kazi kutokana na ushirikiano baina ya wananchi na wanakamati hali iliyoleta tija katika kuandika taarifa hiyo tuliyoiwasilisha serikalini,"alisema Diwani huyo.


Pia alisema wanamshukuru waziri mkuu kwa kupokea taarifa hiyo na kuwaahidi kupitia Mbunge wa Ngorongoro kuwa serikali itarudi kwa ajili ya majadiliano  hivyo wanategemea taarifa hiyo kutoa mateokeo chanya.

Pamoja na hayo changamoto zinazoelezwa ni wingi wa mifugo pamoja na ongezeko la watu kwa mujibu wa serikali ambapo wamesema Ngorongoro wanayoitaka na wanayoiendea kwa miaka elfu ijayo siyo Ngorongoro ya wataalam.









Share To:

JUSLINE

Post A Comment: