Na Ahmed Mahmoud 
Shayiri ni zao la kibiashara lililosahauliwa hapa nchini,ambalo lilisaidia kuendesha viwanda na kuwapa wananchi kipato hususani katika mikoa ya kanda ya kaskazini. 

Kwa muktadha huo ukawa mwisho wa zao la shayiri kuanguka kwa soko lake na wakulima waliobakia kuendelea kuuza katika viwanda hivyo vya Pombe bila kuwa na uhakika wa soko na Zao hilo kununuliwa nje ya nchi na taasisi hizo hususani Afrika ya Kusini. 

Ulimwaji wa zao hilo ulilimwa zaidi katika maeneo ya Wilaya za Siha Karatu na Monduli katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambapo kwa Sasa zao hilo hulimwa katika maeneo mawili pekee. 


Katika miaka ya 2003 wakati huo serikali ikibinafsisha mashirika ya umma ndipo mashamba haya ya shayiri yaliuzwa mfano maeneo ya Londrose wilayani Siha kulikuwa na mashamba ya makubwa yakimilikiwa na TBL ndio kifo chake kiliishia hapo. 

Waandishi wa habàri watafiti na wabunifu waliopatiwa mafunzo ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wameambiwa kwamba kituo cha TARI-Selian kinakuja na Utafiti wa uboreshaji wa mbegu za zao hilo kukuza upatikanaji wake na kuuzwa nje ya nchi. 


Akiongea na wanahabari hao watafiti na wabunifu kuandika habàri za kiutafiti kwa lugha rahisi Mtafiti Salome Munissi ambaye ni mratibu wa zao la Shayiri Kitaifa amesema shayiri ni zao linalolimwa hapa nchini kwa ajili ya kutengeneza Bia tofauti na ngano. A

Aidha amesema kuwa kwa jitihada za TARI seliani wameshapata Tani 1379 za mbegu hizo na kuongezewa thamani ili ziweze kuwa nyingi na wadau waweze kununua mbegu na kuweza kuzisambaza ili wakulima walime shahiri bora zilizofanyiwa tafiti kutoka TARI Seliani. 
Anaeleza zao hilo mbegu yake hununuliwa nje ya nchi hali inayofanya TARI seliani kuendelea kujielekeza kwenye tafiti ya zao hilo zaidi ili kutengeneza mbegu zitakazopatikana hapa nchini zenye ubora unakidhi viwango vya kimataifa. 

Ameongeza kuwa utafiti wanaofanya ni kupata mbegu bora ya shayiri itakayo endana na soko la sasa,kwamba soko la Shahiri kama limetupwa na halina msimamo, hali inayowapa wakulima changamoto ya kuendelea kujiwekeza kwenye zao hilo pendwa duniani. 

Kwa mujibu wa mtafiti Munissi anabainisha kwamba soko la Shahiri pamoja na watafiti wenzake waliwahi kutembelea TBL na Serengeti ilikuzungumza kwa pamoja na kuona ni namna gani watapanua wigo wa soko la uhakika na kupata mbegu za zao hilo hapa bila kutumia gharama kubwa. A


Anasema kwamba zao hilo pendwa lakini hapa nchini hawajui matumizi yake tofauti, na kuuza kwaajili ya utengenezaji wa pombe linahitaji msukumo kuweza kulirudisha katika uhalisia wake ili kuacha kuagiza nje ya nchi. 

 "Shayiri limekuwa zao lililosahauliwa nchini kwa wakulima wengi kukimbilia zaidi zao la Ngano tofauti na huko miaka ya nyuma viwanda vyetu vya pombe walikuwa wakulima na kupata malighafi hapa nchini ila Sasa soko ni dogo ndio maana tumekuja na mikakati huu" 
Salome anaitaka serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)kuja na mkakati mpya utakaosaidia kuongeza thamani ya zao hilo kwa kuzalisha mbegu nyingi zaidi. 


"COSTECH wanao wajibu mkubwa wa kutoa fedha za kuendeleza Utafiti wa mbegu za zao hili kwa kuwa halina wafadhili kutoka nje ya nchi ili kuendelea kuliboresha na kutatua changamoto zake kwa wakulima kupenda kulima zao hilo"anasisitiza Salome.

NUKUU Shayiri ni zao la nafaka, linalotokana na nyasi zikuazo kwa mwaka‘Hardeum vulgare’ shayiri hutumika hasa kulishia mifugo huku kiasi kidogo kikitumika kutengenezea vileo(Bia na vinywaji vingine) na kwenye chakula chenye nguvu.

Shayiri hutumika kwenye supu michemsho na mikate katika nchi mbalimbali kama vile uskochi na Afrika.

Kwa upande wa Tanzania, zao hilo linalimwa katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara baada ya kampuni mbalimbali zinazotengeneza pombe kujitokeza kuwahamasisha wakulima ili waweze kulima zao hilo kwa kilimo cha mkataba.NUKUU ya zao hilo, takwimu zilizotolewa mwaka 2007, kulingana na takwimu za mazao ya nafaka duniani, shayiri lilikuwa zao la nne kwa wingi wa tani milioni 136, likichukua kilomita za mraba 560,000 katika eneo la uzalishaji.

Inaelezwa kibaiolojia mmea wa shayiri ni miongoni mwa familia ya nyasi, hujichavusha wenyewe, wenye kromosomu 14 wakati binadamu ana kromosomu 38 kwa ulinganishi tu.


Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: