MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) imetangaza bei mpya za nauli za mabasi na daladala nchini.



Akitangaza kiwango hicho kipya cha nauli leo Aprili 30, 2022 Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema kiwango hicho kipya kitaanza kutumika baada ya siku 14.

Bw.Ngewe amesema nauli za daladala kuanzia kilomita 0-10 nauli itakuwa shilingi 500 kutoka sh.400 na kilomita 11-15 nauli itakuwa sh. 550 kutoka sh. 450 na bei ya mwisho ya daladala kwa kilomita 36 hadi 40 itakuwa sh.1,100 kwa daladala tu.

Kwa upande wa nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda kwa daraja la kawaida ni sh. 41.29 kwa kilomita moja kutoka sh. 36.89 huku daraja la kati likipanda kwa shilingi 56.88 kutoka sh. 53.22 ambapo nauli kwa wanafunzi imebakia kuwa sh.200 kwa daladala
Share To:

Adery Masta

Post A Comment: