Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde leo amekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Tsh 5,100,000 kwa ajili ya zahanati ya Mtaa wa Ngh’ambala,Chigongwe Jijini Dodoma.


Fedha hizo ni sehemu ya utekelezaji wa miradi chini ya mfuko wa Jimbo Dodoma Mjini ambayo imejikita katika maeneo ya Afya na Elimu.


“Zahanati hii ikikamilika itasaidia sana kuwapunguzia mwendo wananchi wa Ngh’ambala kutembea umbali mrefu kufuata huduma.


Zaidi ya wananchi 3000 watanufaika na huduma za Afya kupitia zahanti hii,na hivyo kusaidia kuboresha huduma za Afya kama inavyoelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Zahanati hii tumeianza kuijenga mimi na ninyi kwa nguvu zenu,na najua Serikali itatuunga mkono katika hatua iliyobaki.Nitahakikisha tunasimamia zahanati hii ianze kutoa huduma mapema iwezekanavyo”Alisema Mavunde


Naye Diwani wa Kata ya Chihongwe  Machela amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna anavyojitoa kutatua changamoto za wananchi katika eneo hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana nae bega kwa bega katika kuwahudumia wananchi.

Share To:

Post A Comment: