Na Mwandishi Wetu

April 29, 2022 Kampuni namba moja kwa utoaji wa huduma za kidigitali nchini Tanzania Tigo , imefunga safari kumfuata mshindi wa droo kubwa ya Millioni 25 promosheni ya Pesa Mwaa Mwii na Tigo Pesa ambaye ni Bi. Suzanne A. Daniel Mkazi wa Kigamboni Jijini Dar Es Salaam.

Bi Suzzanne aliibuka mshindi wa Milioni 25 Aprili 21 , 2022 ambapo Droo ya fainali ilichezeshwa katika ofisi za Tigo makao Makuu Jijini Dar Es Salaam, Mbali na Bi. Suzzanne walipatikana pia Washindi 10 wa milioni kumi kumi kila mmoja.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi Mshindi Hundi ya Millioni 25  ,Meneja wa Kitengo cha wateja Binafsi Tigo Pesa Bi. Mary Rutta  amewapongeza wateja wote walioibuka washindi wa zawadi mbalimbali na pesa taslimu katika promosheni hii ya PESA MWAA MWII NA TIGO PESA na kuwasihi wateja wengine ambao hawakubahatika kushinda kuendelea kutumia Tigo Pesa maana kuna mambo mengi na mazuri yanakuja

" Kama ilivyo kawaida yetu Tigo Pesa hatujawahi kuishiwa  kutoa zawadi na mambo mengine mazuri kwa wateja wetu , Leo tunamkabidhi Mshindi wetu mkubwa wa promosheni yetu Bi. Suzzanne zawadi yake ya Million 25 lakini niwasihi wateja wetu kuendelea kutumia huduma zetu maaana kutumia Tigo Pesa kunalipa " .

Kwa upande wake , Suzanne Assey Daniel , Mama Ntilie ( miaka 41 ) amewapangeza sana Tigo Tanzania kwa kuwajali wateja wake na kuamua kuwarudishia fadhila kupitia promosheni mbalimbali

" Kwakweli sikuamini baada ya kupigiwa simu na kuambiwa kwamba nimeshinda milioni 25 kutoka promosheni ya Pesa Mwaa Mwii , nilihisi kama muujiza lakini namshukuru Mungu leo nakabidhiwa Milioni 25 ambazo zitanisaidia kuongeza biashara yangu ya uuzaji wa chakula , Mungu awabariki sana Tigo hakika nimeamini kutumia Tigo Pesa kunalipa nawasihi watanzania wasizipuuuze promosheni mbalimbali zinazotangazwa na Tigo huenda wakawa wenye bahati na wakabadilishiwa maisha yao kama ambavyo leo Tigo wanaenda kubadilisha maisha yangu ". Alimalizia Bi. Suzzanne

Kumbuka walioibuka washindi kwenye promosheni hii ya PESA MWAA MWII NA TIGO PESA ni waliofanya miamala mara nyingi kupitia huduma za Tigo Pesa ikiwa ni pamoja na Lipa Kwa Simu, Malipo ya Bili, Malipo ya Serikali, miamala ya mtandaoni kutoka kwa wenzao na kupokea pesa kutoka kwa mtandao mwingine wa simu .

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: