Na Prisca Libaga Maelezo Arusha.

MAABARA ya  kisasa yawezesha kuongezeka uzalishaji wa mbegu za matunda,mbogamboga,miche ya migomba na.viungo ili kuondoa changamoto iliyokuwepo ya upungufu wa mbegu bora.


Mkuu wa maabara ya kituo cha utafiti wa mboga mboga na Matunda, TARI,kilichopo Tengeru,wilayani Arumeru,Fatuma Kilua,anasema upatikanaji wa maabara ya kisasa kumewezesha kumaliza changamoto iliyokuwepo ya upungufu wa mbegu ambao uliwaathiri wakulima kushindwa kufikia malengo ya uzalishaji.



Anasema kuwa taasisi hiyo ilipata ufadhili kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, COSTECH, kumeiwezesha taasisi hiyo kusimama kifua mbele kutokana na kuongeza uzalishaji wa mbegu na miche na kusambaza mahitaji ya walengwa.


Kilua, anasema kabla ya kupata ufadhili huo walikuwa hawatoshelezi mahitaji ya wakulima ya kupata mbegu bora za kisasa ambazo zina zaa sana hazishambuliwi na wadudu wala magonjwa.



Anasema taasisi hiyo inazalisha mbegu na miche kwa kutumia teknolojia ambayo inawezesha kupatikana mbegu zenye ubora zinazohimili magonjwa na wadudu hivyo inakuwa ni taasisi ambayo inategemewa na mkombozi kwa mkulima .


Fatuma,anasema kuwa hivi sasa maabara hiyo inazalisha mbegu na miche kwa kutumia teknolojia ya chupa ambapo wanazalisha mbegu za viungo,migomba matunda na mbogamboga.


Anasema kuwa maabara hiyo inao wataalamu wa kutosha hivyo  ina uwezo wa kuzalisha na sasa  inawaomba wa kulima wanaohitaji kupata mbegu na miche ya matunda kufika kituoni hapo ili kupata mahitaji ya kile wanacho kihitajia
Ufadhili huo kutoka COSTECH,umeiwezesha maabara hiyo kuzalisha miche ya migomba 20,000 kwa teknolojia ya chupa kwa awamu moja kwa mwaka  lengo ni kueneza migomba ya kisasa kwa  wakulima.


Mtafiti msaidizi William Mgale,kitengo cha uzalishaji wa miche ya miti ya kivuli ,miche ya matunda vipando vya mpera,pasheni papai mananasi na udongo.

Anasema kutokana na kukua kwa teknolojia wanazalisha Parachichi.kwa ajili ya mikoa ya Ukanda wa joto ikiwemo Dar es Salaam Zanzibar na Pwani.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: