Julieth Ngarabali. Pwani,


 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdurahamani Kinana amewaonya wanachama wa Chama hicho wanaotumia njia zisizokubalika ikiwemo fedha ili kuchaguliwa waache kwa sababu chama hakitawavumilia kwa kua ni kinyumr na kanuni zilizopo


Kinana ametoa onyo hilo  Wilaya Mkuranga Mkoani Pwani huku kukiwa tayari michakato mbalimbali ya uchaguzi imeanza katika ngazi mbalimbali nchini kote


"Uchaguzi unaendelea hadi mei 15 mwaka huu katika ngazi mbalimbali na ngazi za chini ndiko ziliko nguvu za Chama kwenye matawi Kata na Wilaya sasa ni vema tuwe makini Ili tupate viongozi wa kweli"amesema Kinana na kuongeza


"Utakuta mtu hajawahi kuwatembelea wananchi na wala hana nia yakweli ya uongozi lakini anajitokeza wakati wa uchaguzi kuomba nafasi kwakutumia pesa au maneno ya kumharibia mtu mwingine Ili asichaguliwe hilo watu wa aina hiyo msiwakubali majina yao leteni ".


Kinana amesema kazi ya CCM ni kuwasikiliza wananchi, kuwasemea na kuwasaidia juu ya changamoto walizonazo na si kuangalia maslahi binafsi na pia amewataka viongozi kuwa makini na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kufuata misingi iliyopo na kama mtu atabainika kupata nafasi kwa njia za udanganyifu taratibu zifuatwe.


"Kama kuna mtu ataona kuwa ameonewa kuna maeneo ya kupeleka malalamiko kwakufuata utaratibu lakini ni vema uchaguzi ufanyike kwa kufuata taratibu zilizopo"alisema.


Kuhusu ombi la Mmoja wa viongozi wa ngazi za matawi kulipwa posho lililowasilishwa na Mmoja wa viongozi  Mwajuma Nasoro,   Kinana amesema huo utaratibu ulikuwepo hivyo atafuatilia Ili suala hilo lifanyiwe kazi.


Akisoma taarifa ya CCM Pwani, katibu wa chama hicho mkoani humo Saidi Goa amesema Chama hicho hivi sasa pamoja na mambo mengine kina mipango wa kuboresha vitega uchumi Ili kuepukana na misaada yenye masharti.


"Tunampango wa kukamilisha Ujenzi wa uwanja maeneo ya sabasaba Kibaha na ukumbi wa Mkutano na sherehe ambazo zitakuwa zinatuingizia kipato cha uhakika"amesema Goa


Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amebainisha  katika mipango ya kuboresha sekta mbalimbali Mkoa huo umeweza kurejesha jumla ya wanafunzi 269 waliokuwa wamekatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito.


Kunenge ametaja mafanikio ni pamoja na kuendelea kutoa elimu bila malipo ambapo  kwa kipindi cha mwaka 2021 jumla ya sh. Bil 8. 72 zilipokelewa huku mwaka 2021/2022 hadi kufikia Februari tayari sh, Bil .6.94 zilitolewa na zinatafaisha wanafunzi 483,128


"Mheshimiwa Makam Mwenyekiti hii sasa inajibu hoja na tetesi ya upotoshaji uliokuwa unasemwa kwamba Serikali sasa haisomeshi, haitoi fedha lakini sisi tunawahakikishia kwamba Serikali inaendelea kufanya jukumu hili"amesema Kunenge.


Kuhusu maswala ya uchumi  Kunenge amebainisha mpaka sasa Mkoa una jumla ya viwanda 1453 ambavyo vimeongeza ajira na kukuza uchumi na mpaka sasa wameendelea kutenga maeneo ya uwekezaji.


Aidha Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega amemuomba Kinana kuwasilisha kwenye vikao vya ngazi za juu ombi la wakazi wa Wilaya hiyo juu ya upanuzi wa barabara ya kutoka Daresalaam kuelekea mikoa ya kusini kuwa ya njia nne Ili kupunguza adha ya foleni ambayo wamekuwa wakiipata.

Share To:

Post A Comment: