Na Prisca Libaga Maelezo Arusha




Imeelezwa kwamba  Miradi iliyofadhliwa na Tume  ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imefanikiwa na kuleta matokeo chanya katika sekta za Utafiti na Ubunifu.


Akiongea na wanahabari Mara baada ya mafunzo kwa wanahabari wa kanda ya kaskazini watafiti na wabunifu yaliondaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)mratibu Leonard Deusdedit amesema kumekuwa na matokeo chanya.


Amesema kwamba Miradi mingi tuliofadhili imeonyesha matokeo chanya hususani miradi inayopewa kipaumbele na serikali na kwamba sio kila ubunifu unaoletwa kwetu.


Aidha COSTECH imeendelea kufadhili miradi hiyo ya Ubunifu na Utafiti kwa Lengo la kukuza Sayansi Teknolojia na Ubunifu katika kuhakikisha tafiti zinapata nafasi ya kumnufaisha mwananchi na Taifa.


"Miradi mingi ya Utafiti imeleta mafanikio ni Jambo la kujivunia sana ukiangalia utaona kama huyu kijana alileta mashine na tukampa fedha Leo anauwezo wa kutengeneza hadi mashine ya kupukuchua nafaka"


Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Imara Tech Alfred Chengula ameendelea kuishukuru COSTECH kwa ufadhili wanaotoa kwao ambao umewasaidia kuongeza uzalishaji.


Amesema kwamba Serikali hususani viongozi wawe karibu na watafiti na wabunifu ili kuweza kujua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ufinyu wa fedha ushirikiano duni na taasisi za kifedha. 


"Kumekuwa na ugumu wa milango mingi ya viongozi kufikika hili limesababisha mashirikiano Kati yetu na serikali taasisi za kifedha kuwa mgumu na kusababisha kutofikia malengo tunayotarajia"

Share To:

Post A Comment: