Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akizungumza na Wajumbe (hawapo pichani) ambao watakuwa washauri wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya ya Mkalama baada ya kuapishwa katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya hiyo leo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega.
Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akimkabidhi hati ya kiapo Mjumbe wa baraza hilo Kitundu Kitundu baada ya kula kiapo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega. akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama, Elizabeth Rwegasira akichangia jambo kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa wilaya hiyo  Baraka Shuma akishukuru kuanzishwa  kwa baraza hilo.

Wajumbe washauri wa  baraza la Ardhi na nyumba wilayani humo kabla ya kuapishwa. Kutoka kushoto ni Charles Makala, Kitundu Kitundu, Hamisi Salim na  Zulfa Mvungi.

Wazee wa baraza la Ardhi na Nyumba kutoka Wilaya ya Iramba waliohudhuria hafla hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa kwenye hafla hiyo.

Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Lillian Kasanga akiwa kwenye hafla hiyo.
Mjumbe wa baraza hilo Hamis Salim akisaini kiapo baada ya kuapishwa. Kulia ni Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Matrider Meckson aliyeongoza shughuli ya kuapishwa kwa wajumbe hao.
Mjumbe wa baraza hilo, Charles Makala akila kiapo.
Mjumbe wa baraza hilo, Charles Makala akisaini kiapo chake.

Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa wilaya hiyo  Baraka Shuma akiteta jambo na Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Matrider Meckson  wakati wa zoezi la kula kiapo  kwa wajumbe hao.
Mjumbe wa Baraza hilo, Hamis Salim akila kiapo.
 

Na Dotto Mwaibale, Mkalama

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida imeingia katika historia baada ya kupata wajumbe watakaokuwa wakishauri na kusikiliza migogoro ya ardhi na nyumba huduma ambayo haikuwepo tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo mwaka 2015.

Kupatikana kwa wajumbe hao na kuanza kusikiliza migogoro hiyo ya ardhi kutawapunguzia adha waliokuwa wakiipata wananchi wa wilaya hiyo ya kutembelea umbali mrefu kwenda kusikiliza mashauri yao wilayani Iramba hali iliyosababisha baadhi yao kupoteza haki zao kwa kukata tama ya kwenda kusikiliza kesi kutokana na umbali huo.

Akuzungumza leo baada ya kuapishwa kwa wajumbe hao ambao watakuwa washauri wa baraza la ardhi na nyumba wilayani humo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge aliwataka waende kutenda haki wakati wa kutoa maamuzi yao na kujiepusha na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Mahenge aliwataka wajumbe hao kabla ya kuanza kazi hiyo iliyopo mbele yao jambo la kwanza wanalopaswa kulifanya ni kwenda kuzisoma  nyaraka zote zenye maamuzi ya mabaraza yaliyopita ili waweze kuelewa upana na maamuzi mbalimbali yaliyofanyika katika mabaraza hayo.

“ Nawashauri msianze kusikiliza kesi bila ya kujifunza kwa wiki mbili au zaidi namna ya kuzisikiliza na kuzitatua na kujiongeza kusoma mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya utatuzi wa migogoro hiyo ” alisema Mahenge.

Dk. Mahenge aliwataka wajumbe hao waende kutoa maamuzi bila ya kuiga yaliyowahi kutolewa na mtu Fulani bali wajiridhishe baada ya kuyasikiliza na kutoa maamuzi sahihi na si vinginevyo.

Aidha Mahenge aliwaambia wajumbe hao kuwa wana kwenda kutatua kero ya migogoro ya ardhi ambayo ni kubwa mno kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya, kata hadi vijijini hivyo jukumu lao ni kwenda kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuisaidia Serikali.

Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Kizigo alisema kwa muda mrefu wananchi walikuwa wakipoteza haki kwa namna mbili ya kwanza kupindishwa na watoa maamuzi na mbili ni kushindwa kumudu gharama za kwenda kusikiliza mashauri yao wilayani Iramba.

Aliwataka wajumbe hao kwenda kufanya kazi kwa bidii na kuwatahadharisha kutolewa madaraka kwani kumekuwa na tabia ya mtu akipata kazi miezi ya mwanzo anafanya vizuri lakini baada ya muda mfupi hubadilika na kuonesha tabia yake isiyo nzuri hivyo aliwata kuwa makini kwani wanapewa miezi sita ya matazamiao na kubaini kama walichagua wajumbe wazuri au laa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo James John  Mkwega alisema kupatikana kwa baraza hilo kwao ni tunu kubwa hivyo alitumia nafasi hiyo kuipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ofisi ya mkuu wa mkoa, wilaya na viongozi wote walioshiriki kusaidia kupata baraza hilo.

“Tumepata halmashauri hii tangu mwaka 2015 na tuliletewa huduma nyingi lakini huduma iliyokuwa ikitutesa sana ni hii ya utatuzi wa migogoro ya ardhi kwani wanamkalama wengi waliokuwa na kipato  kidogo walipoteza haki zao kwani walipokuwa wakikatiwa rufaa ya mashauri yao kwenda Kiomboi walishindwa kutokana na umbali na gharama hivyo kupelekwa kwa huduma hiyo makao makuu ya wilaya hiyo Nduguti kutatoa fursa kwa kila mwananchi kupata haki yake” alisema Mkwega.

Mkwega aliwaambia wajumbe hao kuwa Wanamkalama zaidi ya 200,000 wamewapa dhamana ya kuwatumikia na kuwa hawahitaji baraza bali huduma hivyo wanaimani nao kubwa watamshauri mwenyekiti wao Baraka Shuma ili waweze kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuhakikisha haki inatendeka kwani  kwa wanamkalama hakuna utajiri mkubwa kama ardhi hivyo ilkilindwa ardhi hiyo ambayo wamezoea kurithishana kwa utamaduni wao hata kwa Mwenyezi Mungu watabarikiwa. 

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Baraka Shuma alishukuru kuanza kwa baraza wilayani humo na kuwa kulikuwa na changamoto kubwa kwa wananchi ya kupata huduma kwa kutembea umbali mrefu kuifuata  Kiomboi Iramba hasa kipindi cha mvua za masika.

Alisema baraza hilo litaanza kufanya kazi wakati wowote baada ya idadi ya wajumbe wasiopungua wawili kukamilika akiwepo Mwenyekiti na kula kiapo mbele ya mkuu wa mkoa husika na kuwa jambo hilo ni la kihistoria katika wilaya hiyo.

Wajumbe hao washauri wa  baraza la Ardhi na Nyumba walioapishwa ni Charles Makala, Kitundu Kitundu, Hamisi Salim na  Zulfa Mvungi.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: