Na John Walter-Manyara

Mwili wa Mtoto wa kike anaekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 11 hadi 13 ambaye jina lake halijatambulika wala anapotoka, umeokotwa ukiwa umenasa kwenye tope katika mto Faheri uliopo mtaa wa Hangoni C mjini Babati.

Hayo yameelezwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga wakati alipokuwa akizungumza na kituo hiki ofisini kwake.

Kamanda kuzaga amesema mpaka sasa mtoto huyo hakuna taarifa walizozipata kuhusu ndugu au mzazi anayemtafuta na kwamba mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospital ya mji wa Babati Mrara.

Katika tukio lingine kamanda Kuzaga amesema watu watatu wamekufa katika matukio tofauti ikiwemo mwanafunzi mwenye umri wa miaka 10 Siamoi Yona baada ya kushambuliwa na mnyama Mamba akiwa anaogelea kwenye mto Ruvu uliopo wilaya ya Simanjiro.

Aidha amesema katika kijiji cha Dareda kata ya Ayalagaya tarafa ya Bashnet wilaya ya Babati mkulima wa Bacho B Dareda kati aligundua mabaki ya mwili wa binadamu ambaye bado hajafahamika, yakiwa katika shamba la Hando Baso huku ikisadikika kuwa mtu huyo huenda ameliwa na mnyama aina ya fisi baada ya kulewa pombe.

Taarifa ya kamanda Kuzaga imeeleza kuwa Machi 16,2022 ndani ya ziwa Babati kata ya Bagara mtu aliyefahamika kwa jina la Petro (50) mkazi wa kigongoni alikutwa akiwa amefariki baada ya kushambuliwa na Mnyama Kiboko akifanya shughuli za uvuvi kwa kutumia Mtumbwi ziwani hapo.

Mwanafunzi wa darasa la pili Anayeitwa Siamoi yona (10) anayeishi kijiji cha ngage kata ya Lobosoit (B) wilaya ya simanjiro Mkoa wa Manyara,  amefariki dunia baada ya kushambuliwa na mnyama Mamba wakati akiogelea katika mto Ruvu uliopo wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Manyara ACP Benjamine Kuzaga amesema tukio hilo limetokea siku ya tarehe 13/03/2022 huko katika mto Ruvu.

Aidha kamanda Kuzaga amesema yapo matukio mengine yaliyotokana na maafa ambapo yupo mtoto mwingine Binti ambaye hajatambulika kwa majina na umri wake unakadiriwa kati ya miaka 11 Mpaka 13 ambapo  alisobwa na maji yanayotokana na Mvua zinazoendelea na hatimaye kupoteza maisha.

Pia tukio jingine ni la mtu Mmoja aliyeuwawa kwa kushambuliwa na boko katika ziwa Babati wakati akifanya shughuliza za uvuvi katika ziwa hilo,  ambapo tukio hilo limetokea siku ya tarehe 16/03/2022 katika eneo la kata ya Bangara wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara.

Kamanda Kuzaga amesema aliyeuwawa na Kiboko ni Petro Elias sabuni (50) mkulima na mkazi wa kigongoni,  ambapo alikutwa akiwa amefariki baada ya kushambuliwa na Kiboko wakati akifanya shughuli za uvuvi ndani ya ziwa Babati kwa kutumia Mtubwi wake.

Aidha katika tukio jingine nipamoja na mtu Mmoja amefariki dunia mara baada ya kushambuliwa na fisi katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku mabaki ya mwili wake yamekutwa katika shamba la Hando katika kijiji cha Dareda kata ya Ayagala wilayani Babati mkoa wa Manyara.

Kamanda kuzaga amesema tukio hilo limetokea siku ya Tarehe 24/02/2022 ambapo January Flavian (56) mkulima wa kijiji cha Bacho (B) Dareda kati aligundua mabaki ya mwili wa  binadamu ambaye mpaka sasa hajafahamika ambapo mabaki hayo yalikuwa katika shamba la Hando Baso na inasadikika kuwa mtu Huyo ameliwa na Mnyama aina ya fisi baada ya kulewa.

Hata hivyo jeshi la polisi Mkoa wa Manyara limetoa wito kwa wananchi wote kuchukuwa tahadhari juu ya majanga yanayotokana na Mvua pamoja na mengine ambayo yanaweza kuhepukika ili kuokoa maisha juu ya majanga hayo.

Share To:

Post A Comment: