Katibu Mkuu UVCCM Ndg. Kenani Kihongosi, aongoza Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 19/3/2022 katika Uwanja wa Taifa Kahama, Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
Leo Tarehe 19 Machi 2022 alipiga simu kuzungumza na vijana katika kongamano la kuadhimisha mwaka mmoja wa Kishindo wa Serikali ya Awamu ya sita kupitia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana ndugu Kenani Kihongosi

Amewapongeza na kuwashukuru vijana  kwa mchango wao katika siku 365 za Serikali ya awamu ya sita na kuwasisitiza juu ya kulinda Amani na utulivu.

"Niwaombe sana tuendelee kulinda Amani na utulivu, tuchape kazi, tufanye siasa za kistaarabu. Vijana ninyi ndio nguzo yangu nawategemea sana"

Kongamano hilo limefanyika Wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama, Jumuiya na Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mh Festo Kiwaga, Wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM TAIFA, Wenyeviti na Makatibu wa Chama na Jumuiya.















Share To:

Post A Comment: