Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali,Emmanuel Tutuba amewataka wajumbe wa Baraza la Chuo cha Uhasibu Arusha kuzingatia Sheria,Kanuni,Taratibu na Miongozo ili kukiweka chuo hicho katika hadhi nzuri.



Tutuba ametoa wito huo wakati akizinduzi baraza la uongozi la Chuo cha Uhasihu Arusha ambapo amewataka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha wanaepuka migogoro ya ndani na nje ya chuo na kuweka mazingira vizuri itakayoondoa mivutano ili kulinda hadhi ya chuo hicho isishuke.


"Kwa kipindi ambacho mmepokea jukumu hili watangulizi wenu waliweza kuyafanya mengi mpaka hapa kilipofikia,kwahiyo mnapopokea chuo hiki mfahamu kwamba mnao wajibu wa kuendelea kudumisha mazuri yaliyotangulia kuongeza ubunifu mkubwa zaidi ili kuleta tija na ufanisi."Alisema Tutuba



Aidha amesema katika taasisi kama hizo zinakuwa na muunganiko wa masuala mengi yenye lengo la kuhakikisha chuo kinaendelea kushamiri kwa kutoa wahitimu wenye maadili,viwango na weledi unaotakiwa katika soko la ajira na kuweza kudumisha mazuri yaliyotangulia ,kuongeza ubunifu  sambamba na kukifanya chuo hicho kuweza kuleta mchango mkubwa kwenye tasnia ya masomo yanayofanyia.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Dkt.Mwamini Ntuli amesema Wizara ya fedha na mipango kama mlezi imesaidia kukilea chuo hicho  kwa kutoa maelekezo na miongozo mbalimbali ambapo pamoja na wingi wa changamoto zinazowakabili wameiomba wizara hiyo kuwapatia mkopo wa kuweza kumalizia miundombinu ambayo tayari imeshaanzishwa .



Pamoja na hayo amesema kumekuwepo na ongezeko la wanafunzi 9870  kwa kipindi cha miaka 3 iliyopita ambapo uwezo wa chuo ni kulaza wanafunzi ulikuwa 750 na kusema kuwa ujenzi wa hostel hiyo utasaidia kupunguza changamoto za uwepo wa wanafunzi waishio nje ya chuo.






Naye Kaimu Mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha Dkt.Cairo Mwaitete amesema kuwa chuo hicho kimeanzisha IAA PRESS  ambayo inafanya machapisho mbalimbali lengo ni kuifikia jamii na Studio iliyoko katika maboresho sambamba na kuwepo kwa kitengo maalum cha kuibua vipaji vya vijana na kulea mawazo yao ambapo zaidi ya vijana 200 wameweza kusaidiwa kwa kipindi kilichopita. I

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: