Na,Jusline Marco:Arusha


Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha Hargeney Chitukuro amesema sera ya serikali pamoja na kuainisha utoaji wa elimu bure kuanzia kidato cha kwanza hadi kidayo cha nne,imeboresha miundombinu ya elimu ili kuwawezesha watoto wote wanaotakiwa kwenda shule waweze kwenda shule.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo imeadhimishwa na Taasisi lisilo la kiserikali la Umoja Tanzania kwa kushirikiana na shirika Iyanna Foundation,Future stars academy,Tanzania rugby development pamoja na Yes Tanzania ya jijini Arusha.


Chitukuro amesema kipitia sera hiyo pia inatoa umuhimu kwa mtoto wa kike kutorudi nyuma ambapo serikali ya Mkoa wa Arusha inaunga mkono sera hiyo pamoja na kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ambapo amesema serikali kupitia halmashauri imekuwa ikitenga fedha asilimia 10 kati ua hizo asilimia 4 zimekuwa zikitolewa kwa vikundi vya wanawake.


"Hawa vijana wakiweza kikuzwa vizuri na kulelewa kwenye vikundi wakapata elimu ya ujasiriamali wanaweza kutumia fursa ya fedha zinazotengwa kutoka kwenye halmashauri asilimia 4 kwaajili ya vijana wanaweza wakafanya jambo likawasaidia katika maisha."alisema Chitukuro


Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha Hargeney Chitukuro akimvisha medali mmoja wa washiriki wa mchezo wa mbio aliyeshika nafadi ya kwanza katika mbio zilizoambatana na muendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani.


Aidha amesema matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili kwa wanawake na watoto yatakoma endapo jamii itashirikiana na mashirika binafsi katika kupunguza kama siyo kutokomeza kabisa.


Vilevile amelipongeza shirikia hilo kwa kuadhimisha siku hiyo kwa kushirikisha watoto wa kiume kutomana na umuhimu wao katika jamii ambapo amewataka vijana hao kutojiusisha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii pamoja na kufahamu athari za madawa ya kulevya.


"Mitandao hii ya kijamii ni mizuri lakini tunahitaji kuitumia kwa usahihi ili isiweze kuleta madhara na tumeona watu ambao wanaharibika kwa uvutaji wa bangi,unywaji wa pombe kupindukia."alisisitiza Chitukuro


Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Taasisi ya Umoja Tanzania Bi.Chuki Issa katika maadhimisho hayo yamelenga kuwajengea uwezo kuanzia nafasi ya mtoto wa kike oli kumuandaa kuwa na ujasiri ili aweze kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo anaweza kukutana nazo.


Afisa ustawi wa jamii Taasisi ya Umoja Tanzania Bi.Chuki Issa akizungumza katika maadhisho ya Siku ya mwanamke Duniani ambayo yameadhimishwa na baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Arusha


Amesema ushirikishwaji wa watoto wa kike na wakiume katika maadhimisho ni ili kutokomeza masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ambapo amesema taasisi hiyo inamsaidia mtoto wa kike kumpatia elimu na kutoa mafunzo ya jinsia kwa mtoto wa kike kwa kumpa elimu ya masuala mbalimbali ikiwemo uwezo wa kujitambua na namna ya kukabiliana na changamoto tofauti tofauti.


Sambamba na hayo amesema kumjenga mtoto wa kike ni suala la kila mmoja na kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya kikatili na unyanyasaji wa kijinsia ni jukumu la kila mtanzania kuweza kumsaidia mtoto wa kike na kutoa taarifa kwa vyombo husika.


Mmoja wa waandaaji katika maadhimisho hayo Prisca Ephate Lema amesema wataendelea kushirikiana na mashirika mengine katika kukuza vipaji vya watoto wa kike na kuwaongoza katika njia ambazo zitaweza kufikia na kupata ndoto zao na kuepuka changamoto ambazo zinaweza kukatiza ndoto zao kama vile mimba za ndoto zao,kudanganywa pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya kijamii.Mmoja wa waandaaji katika maadhimisho hayo Prisca Ephate Lema ambaye pia ni Mkurugenzi wa Iynna Foundation akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Arusha.
Share To:

JUSLINE

Post A Comment: