Katibu Tawala Msaidizi upande wa Uchumi  na Uzalishaji Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji  akifungua kikao kazi cha kupeana uelewa wa shughuli za udhibiti wa bidhaa za Tumbaku kati ya TMDA, Uongozi wa Wafanyabiashara na  Viongozi wa ngazi ya ya mkoa na Manispaa ya Singida 

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA)  Kanda ya Kati Sonia Mkumbwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho.
Mkaguzi  wa dawa TMDA, Riziki Shemula akitoa mada kwenye kikao hicho.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA)  Kanda ya Kati Sonia Mkumbwa akisisitiza jambo kwenye kikao hicho..

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Taswira ya mafunzo hayo.

Maafisa wa TMDA wakiwa kwenyemafunzo hayo.


Washiriki wakifuatilia mada.


Kikao kazi kikiendelea.

Mada zikiendelea.

Mada zikiendelea.


Washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Mkaguzi wa dawa Saraphiana Cleophace akitoa mada kuhusu udhibiti wa bidhaa za Tumbaku.

Washiriki na mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja.

Washiriki na mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja.
Washiriki na mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja.
Washiriki na mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja.
Washiriki wa mafunzo kwa watumishi wa Sekta ya Afya mkoani hapa yaliyohusu  utoaji wa taarifa za madhara au matukio yanayohisiwa kusabibishwa na Matumizi ya Dawa,Vifaa Tiba,Vitendanishi na Chanjo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

 

Na Dotto Mwaibale, Singida


MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) imepiga marufuku  kutumia bidhaa za tumbaku katika maeneo yasiyo rasmi ili kulinda afya za jamii.

Agizo hilo lilitolewa katika kikao kazi cha kutoa uelewa wa  Udhibiti wa Bidhaa za Tumbaku kilicho wakutanisha TMDA, Uongozi wa Wafanyabiashara na  Viongozi wa ngazi ya  mkoa na Manispaa ya Singida.

Akizungumza kwenye kikao hicho Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Kati Sonia Mkumbwa alisema ni jambo zuri kwa watumiaji wa bidhaa za tumbaku kutengewa maeneo maalumu ya matumizi ya bidhaa hizo ili kuondoa matumizi hayo maeneo ya hadharani ili kusaidia kulinda afya za watu wengine ambao hawatumii  tumbaku.

“Ni vizuri sasa watumiaji wa bidhaa za tumbaku (wavutaji wa sigara) kutengewa maeneneo maalumu ya kutumia bidhaa hizo ambazo zitawekwa vibao vikavyoyaonesha maeneo hayo ili iwe rahisi kutambulika badala ya hivi sasa ambapo matumizi yake yamekuwa yakifanyika hadharani ” alisema Mkumbwa.

Katibu Tawala Msaidizi upande wa Uchumi  na Uzalishaji, Lanslaus Choaji  Mkoa wa Singida akizungumza  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati akifungua kikao kazi hicho  alisema mafunzo hayo ni ya muhimu sana.

Choaji alitumia nafasi hiyo hiyo kuwakaribisha na kuwashukuru wadau wote  kwa kuweza kuhudhuria kikao hicho  muhimu chenye lengo la kupeana uelewa wa shughuli za udhibiti wa matumizi ya bidhaa za tumbaku katika mkoa  wa Singida Pamoja na utekelezaji wake unaofanyika nchi nzima.

“Nafahamu kuwa TMDA imekasimishwa jukumu hili la udhibiti wa matumizi ya bidhaa za tumbaku na Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya Afya  Aprili 30, 2021. Hivyo basi, nawapongeza sana kwa kulipokea jukumu hili na bila kuchelewa mmeweza kuandaa mpango kazi wa miaka mitatu 2021/2022 hadi  2023/2024) wa utekelezaji wa shughuli za udhibiti wa bidhaa hizi lengo likiwa ni kupunguza ama kuzuia matumizi ya bidhaa za tumbaku na madhara makubwa ya kiafya yanayoweza kusababishwa na matumizi ya bidhaa hizi” alisema Choaji.

Alisema tafiti zinaonesha matumizi ya bidhaa za tumbaku yamekuwa yakiongezeka kwa kasi ulimwenguni ambapo chimbuko lake ikiwa katika nchi zilizoendelea lakini kwa sasa imebanika kuwa matumizi makubwa ya bidhaa hizi yako katika nchi zinazoendelea.

“Takwimu zimebainisha kuwa zaidi ya watu bilioni 1.3 ya watumiaji wa bidhaa za tumbaku duniani wako katika nchini zetu zinazoendelea. Aidha, tafiti hizo zimebainisha madhara makubwa yaliyoelezwa ni pamoja na vifo vya zaidi ya watu  milioni 7 duniani kila mwaka vinavyosababishwa na magonjwa yanayotokana na matumizi ya bidhaa za tumbaku.

Wakati huo huo TMDA imetoa mafunzo kwa watumishi wa Sekta ya Afya mkoani hapa yanayohusu  utoaji wa taarifa za madhara au matukio yanayohisiwa kusabibishwa na Matumizi ya Dawa,Vifaa Tiba,Vitendanishi na Chanjo. 

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa awe mgeni rasmi, Elikana Lubango alisema mafunzo hayo yatakwenda kutatua Changamoto kubwa ya utoaji wa taarifa juu ya madhara yanayojitokeza kutokana na matumizi ya dawa. 

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA)  Kanda ya Kati Sonia Mkumbwa amewahimiza Wafamasia kote nchini kuhakikisha wanaingiza au kuuza dawa ambazo zimesajiliwa na TMDA ili kuepusha madhara kwa watumiaji. 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema yatawasaidia katika majukumu yao ikiwa ni pamoja na kutoa huduma nzuri na kuepusha madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba.             

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: